{"id":2876,"date":"2026-07-11T17:05:20","date_gmt":"2026-07-11T15:05:20","guid":{"rendered":"https:\/\/neocatechumenaleiter.org\/evangelizacion\/jumuiya-katika-utume\/"},"modified":"2026-08-26T18:54:57","modified_gmt":"2026-08-26T16:54:57","slug":"jumuiya-katika-utume","status":"publish","type":"evangelizacion","link":"https:\/\/neocatechumenaleiter.org\/sw\/uinjilishaji\/jumuiya-katika-utume\/","title":{"rendered":"Jumuiya katika utume"},"content":{"rendered":"\n<a name=\"comunidadesmision\"><\/a>\n\n\n\n<h3 class=\"has-text-align-center wp-block-heading\">Jumuiya katika utume<\/h3>\n\n\n\n<div style=\"height:20px\" aria-hidden=\"true\" class=\"wp-block-spacer\"><\/div>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Katika\nmkutano na Benedikto XVI katika Basilika la Mtakatifu Petro mnamo Januari 10\n2009, kwa kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 40 ya kuzaliwa jumuiya\nya kwanza ya neokatekumenato huko Roma, zilitumwa na Baba Mtakatifu \n Jumuiya 15 za kwanza kwa maeneo yaliyo nje kidogo ya mji wa Roma.\n<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Jumuiya hizi zilikuwa tayari\nkuacha parokia yao &#8211; ambapo tayari walikuwa wamekamilisha safari\nya neokatekumenato &#8211; ili kwenda kwenye utume kwa maeneo magumu ya nje ya mji kupitia mwaliko wa maparoko. Maeneo yaliyoharibiwa, yenye ukatili mwingi,\nmadawa ya kulevya, familia zilizovunjika, wahamiaji waliowasili hivi karibuni&#8230;\n<\/p>\n\n\n\n<div class=\"wp-block-image is-style-default\"><figure class=\"alignright size-large\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"400\" height=\"267\" src=\"\/wp-content\/uploads\/2022\/12\/Camino_Neocatecumenal_Benedicto_XVI_Kiko_Arguello_envio_misiones_ad_gentes_vaticano.jpg\" alt=\"Kutumwa kwa Missio ad Gentes kutoka Basilika la Mt. Petro\" class=\"wp-image-470\" srcset=\"https:\/\/neocatechumenaleiter.org\/wp-content\/uploads\/2022\/12\/Camino_Neocatecumenal_Benedicto_XVI_Kiko_Arguello_envio_misiones_ad_gentes_vaticano.jpg 400w, https:\/\/neocatechumenaleiter.org\/wp-content\/uploads\/2022\/12\/Camino_Neocatecumenal_Benedicto_XVI_Kiko_Arguello_envio_misiones_ad_gentes_vaticano-300x200.jpg 300w\" sizes=\"auto, (max-width: 400px) 100vw, 400px\" \/><\/figure><\/div>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Kiko,\n  akitambulisha utume huu mpya, alisema kwamba &#8220;Njia inaisha\nkwa kutangaza Injili ulimwenguni kote. &#8220;Moja ya mambo mapya zaidi\n  ni kwamba jumuiya nzima inaenda kwenye utume. Siyo baadhi ya ndugu, jumuiya\nnzima inaenda. Ni neema kubwa sana na ni kitu cha ajabu kwamba Mungu \nawatume kwa utume huu. Ni ajabu kuweza kuondoka, kwamba Bwana akupatie \nutume; kufa katika utume, kuzeeka katika utume.&#8221;\n<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Kwa namna sawia, Papa Fransisko katika barua yake ya <em>Evangelii Gaudium<\/em> anazungumza juu ya Kanisa &#8220;linalotoka nje&#8221; na kuelezea hitaji la kuinjilisha maeneo ya &#8220;nje&#8221;, kijiografia na kimaisha: &#8220;<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Pia jimbo la Madrid, ambapo\nNjia ilizaliwa na ipo katika parokia 45 zenye jumuiya 221,\nyako maang&#8217;amuzi haya. Mwaka 2011, Askofu Mkuu wa Madrid wakati huo, Kardinali Rouco Varela alituma jumuiya 10 za kwanza kwenye utume.\n<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Askofu Mkuu wa sasa wa mji mkuu wa Hispania, Kardinali Carlos Osoro Sierra, katika mkutano wa Machi 22, 2015, alituma jumuiya 8 mpya. Huko Madrid, kuna jumla ya <em>jumuiya 18 katika utume.<\/em><\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Tarehe 5 Mei 2018, Papa Fransisko,\n  katika kuadhimisha miaka 50 ya kuzaliwa kwa jumuiya ya kwanza\nya Njia huko Roma, katika mkutano mkubwa huko Tor Vergata (Roma) alituma \njumuiya 25 kwenye utume kwa parokia mbalimbali za Roma ili kutegemeza na\nkuimarisha maisha ya kikristo ya jumuiya za parokia zenye magumu zaidi.\n<\/p>\n\n\n\n<p class=\"wp-block-paragraph\">Leo, katika &#8216;nendeni&#8217; hii ya Yesu, yamo\nmazingira na changamoto mpya za utume\nwa kuinjilisha wa Kanisa, na sote tumeitwa kwa &#8220;mtoko&#8221; huu mpya\nwa kimisionari. Kila mkristo na kila jumuiya itapambanua ipi ndiyo njia ambayo Bwana anaomba kwake, lakini sote tunaalikwa kukubali\nwito huu: kutoka katika raha yako na kuthubutu kuyafikia maeneo\nyote ya mbali yanayohitaji nuru ya Injili\u201d.\n<\/p>\n\n\n\n<div style=\"height:20px\" aria-hidden=\"true\" class=\"wp-block-spacer\"><\/div>\n\n\n\n<hr class=\"wp-block-separator\" \/>\n\n\n\n<div style=\"height:20px\" aria-hidden=\"true\" class=\"wp-block-spacer\"><\/div>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Jumuiya katika utume Katika mkutano na Benedikto XVI katika Basilika la Mtakatifu Petro mnamo Januari 10 2009, kwa kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 40 ya kuzaliwa jumuiya ya kwanza ya neokatekumenato huko Roma, zilitumwa na Baba Mtakatifu Jumuiya 15 za kwanza kwa maeneo yaliyo nje kidogo ya mji wa Roma. Jumuiya hizi zilikuwa tayari kuacha parokia [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":0,"featured_media":470,"template":"","meta":{"_hide_header":false,"_hide_footer":false,"_nck_seo_title":"","_nck_seo_description":"","footnotes":""},"categories":[],"tags":[],"class_list":["post-2876","evangelizacion","type-evangelizacion","status-publish","has-post-thumbnail","hentry"],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/neocatechumenaleiter.org\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/evangelizacion\/2876","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/neocatechumenaleiter.org\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/evangelizacion"}],"about":[{"href":"https:\/\/neocatechumenaleiter.org\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/types\/evangelizacion"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/neocatechumenaleiter.org\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/evangelizacion\/2876\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":22838,"href":"https:\/\/neocatechumenaleiter.org\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/evangelizacion\/2876\/revisions\/22838"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/neocatechumenaleiter.org\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/media\/470"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/neocatechumenaleiter.org\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=2876"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/neocatechumenaleiter.org\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=2876"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/neocatechumenaleiter.org\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=2876"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}