{"id":48460,"date":"2020-02-29T04:25:36","date_gmt":"2020-02-29T03:25:36","guid":{"rendered":"https:\/\/neocatechumenaleiter.org\/maneno-ya-mapapa\/fransisko\/regina-coeli-malkia-wa-mbingu-ya-papa-fransisko-kwa-utume-nyanjani-huko-roma-7-4-2013\/"},"modified":"2026-03-24T04:23:23","modified_gmt":"2026-03-24T03:23:23","slug":"regina-coeli-malkia-wa-mbingu-ya-papa-fransisko-kwa-utume-nyanjani-huko-roma-7-4-2013","status":"publish","type":"page","link":"https:\/\/neocatechumenaleiter.org\/sw\/maneno-ya-mapapa\/fransisko\/regina-coeli-malkia-wa-mbingu-ya-papa-fransisko-kwa-utume-nyanjani-huko-roma-7-4-2013\/","title":{"rendered":"\u00abRegina Coeli\u00bb (Malkia wa Mbingu) ya Papa Fransisko kwa utume nyanjani huko Roma 7-4-2013"},"content":{"rendered":"\n<h1 class=\"has-text-align-center wp-block-heading\">\u00abRegina Coeli\u00bb (Malkia wa Mbingu) ya Papa Fransisko kwa utume nyanjani huko Roma 7-4-2013<\/h1>\n\n<div style=\"height:20px\" aria-hidden=\"true\" class=\"wp-block-spacer\"><\/div>\n\n<h4 class=\"has-text-align-center wp-block-heading\">Fransisko <\/h4>\n\n<div style=\"height:20px\" aria-hidden=\"true\" class=\"wp-block-spacer\"><\/div>\n\n<p><em>Ndugu wapendwa, habari za asubuhi!<\/em><\/p>\n\n<p>Mwinjili Yohana anatuonyesha, katika Dominika hii ya 4 ya kipindi cha Pasaka, sura ya Yesu Mchungaji Mwema.<br \/>Tukitafakari ukurasa huu wa Injili, tunaweza kuelewa aina ya uhusiano ambao Yesu alikuwa nao na wanafunzi wake: uhusiano unaosimama katika upole, katika upendo, katika kujuana na katika ahadi ya kipaji kisichopimika: \u201cMimi nimekuja,\u201d asema Yesu, \u201cili wawe na uzima na wawe nao tele\u201d (<em>Yn<\/em> 10, 10). Uhusiano kama huo ni kielelezo cha mahusiano kati ya wakristo na cha mahusiano ya kibinadamu.<\/p>\n\n<p>Leo pia, kama ilivyokuwa wakati wa Yesu,&#013;\nwengi hujipendekeza kama &#8220;wachungaji&#8221; wa maisha yetu; lakini &#013;\n  Mfufuka tu ndiye Mchungaji wa kweli anayetupatia uzima tele.&#013;\nNinawaalika nyote kuwa na imani katika Bwana anayetuongoza. Lakini si tu&#013;\nkutuongoza: anatusindikiza, anatembea nasi. Tusikilize neno lake pamoja&#013;\nkwa akili na moyo wazi, ili kulisha imani yetu, kuangaza dhamira yetu&#013;\nna kufuata mafundisho ya Injili.&#013;\n<\/p>\n\n<p>Dominika hii tuwaombee wachungaji&#013;\n  wa Kanisa, maaskofu wote, pamoja na askofu wa Roma, &#013;\nmapadre wote, wote. Hasa, tuwaombee mapadre wa jimbo la Roma, &#013;\nambao nimewapadrisha hivi punde katika basilika ya Mtakatifu Petro. &#013;\nSalamu kwa mapadre hawa kumi na watatu. Bwana na atusaidie sisi, &#013;\nwachungaji, kuwa waaminifu daima kwa Bwana na kuwa viongozi&#013;\nwenye hekima na walioangaziwa kwa ajili ya taifa ambalo Mungu amekabidhi kwetu. &#013;\nNinyi pia, nawaomba mtusaidie: mtusaidie kuwa wachungaji wema.&#013;\nWakati fulani nilisoma kitu kizuri sana kuhusu jinsi taifa la Mungu wanavyosaidia&#013;\n  maaskofu na mapadre kuwa wachungaji wema. Ni maandishi ya&#013;\nMtakatifu Caesarius wa Arles, Baba wa Kanisa wa karne za kwanza za Kanisa.&#013;\nAlieleza jinsi taifa la Mungu wanavyohitaji kumsaidia mchungaji, na aliweka &#013;\nmfano huu: ndama anapokuwa na njaa anaenda kwa ng&#8217;ombe, kwa mama yake.&#013;\n  Ili kunyonya. Lakini ng&#8217;ombe hampi mara moja: inaonekana kwamba&#013;\nanayazuia kwa ajili yake. Na ndama hufanya nini? Anaita na pua yake &#013;\nkatika chuchu ya ng&#8217;ombe, ili maziwa yatoke. Picha nzuri kama nini! &#013;\n&#8220;Hivyo ndivyo&#8221;, anasema mtakatifu huyu, &#8220;mnavyopaswa kuwa pamoja na wachungaji: &#013;\nkubisha daima mlangoni mwao, moyoni mwao, ili wawape ninyi maziwa ya mafundisho,&#013;\nmaziwa ya neema, maziwa ya mwongozo&#8221;. Na ninawaomba, tafadhali,&#013;\nmtusumbue wachungaji, mwasumbue wachungaji, &#013;\nwachungaji wetu wote, ili tuwape ninyi maziwa ya neema, &#013;\nya mafundisho na ya mwongozo. Mtusumbue! Fikirieni juu ya picha hiyo nzuri&#013;\nya ndama mdogo, jinsi anavyomsumbua mama yake ili amlishe.&#013;\n<\/p>\n\n<p>Kwa kumwiga Yesu, kila mchungaji \u201cmara nyingine atakuwa mbele ili kuonyesha njia na kutunza matumaini ya watu -mchungaji lazima wakati mwingine atangulie-, mara nyingine atakuwa tu katikati ya wote pamoja na ukaribu wake rahisi na wenye huruma, na wakati mwingine itambidi kutembea nyuma ya taifa ili kuwasaidia wanaovunjika moyo\u201d ( Wosia wa Kitume <em>Evangelii Gaudium<\/em>, 13).<br \/>Laiti wachungaji wote wawe hivyo! Lakini ninyi mwasumbue wachungaji, ili wawape ninyi mwongozo wa mafundisho na wa neema.<\/p>\n\n<p>Jumapili hii inaadhimishwa <em>Siku ya Kuombea Miito Duniani<\/em>. Katika <em>Ujumbe<\/em> wa mwaka huu nimekumbusha kwamba \u201ckila wito (&#8230;) inahitaji daima kuanzisha mwendo wa kutoka katika wao wenyewe ili kumweka Kristo katikati ya maisha yao pamoja na Injili yake\u201d (Na. 2). Ndiyo maana wakati huo huo wito wa kumfuata Yesu unakuwa kipindi cha kusisimua na cha kujihusisha. Ili itekelezwe, ni lazima daima kuanzisha urafiki wa kina na Bwana ili kuweza kuishi kutoka Kwake na kwa ajili Yake.<\/p>\n\n<p>Tuombe ili pia katika wakati huu vijana wengi wasikie sauti ya Bwana, ambayo daima ina hatari ya kuzamishwa na sauti nyingine nyingi. Tuwaombee vijana: labda&#013;\nhapa, katika uwanja huu, yupo mtu anayesikia sauti hii ya Bwana ikimwita kwa upadre; tumuombee, ikiwa yuko hapa, na kwa ajili ya vijana wote wanaoitwa.&#013;\n<\/p>\n\n<hr class=\"wp-block-separator\" \/>\n\n<p><strong>Baada ya \u201cRegina Coeli\u201d (Tenzi kwa Bikira Maria \u201cMalkia wa Mbingu\u201d, kwa kilatini)<\/strong><\/p>\n\n<p><em>Ndugu wapendwa:<\/em><\/p>\n\n<p>Ninawasalimu ninyi nyote, familia, vikundi vya parokia, vyama na waamini kutoka Italia &#013;\nna nchi nyingi (\u2026).&#013;\n<\/p>\n\n<p>Salamu kwa Jumuiya za Neokatekumenato, &#013;\nambao katika Jumapili hizi za kipindi cha Pasaka wanabeba&#013;\ntangazo la Yesu mfufuka katika viwanja\/nyanja 100 hapa Roma &#013;\nna katika majiji mengi ya dunia. Bwana awape furaha ya Injili! &#013;\nNa songeni mbele, ninyi mliojaa ujasiri!&#013;\n<\/p>\n\n<p>Baraka maalum kwa watoto na vijana wadogo &#013;\nambao wamepokea au wanakaribia kupokea komunyo ya kwanza na&#013;\n  kipaimara. Na pia kwa wanafamilia na marafiki wa mapadre wapya &#013;\nwa jimbo la Roma, niliowapadrisha asubuhi hii ya leo.&#013;\n<\/p>\n\n<p>Na leo ninawaalika kuwatolea kumbukumbu nzuri\/rembo\/nyororo&#013;\nna sala kwa akina mama wote. Tuwasalimie akina mama!&#013;\nTukiwakabidhi kwa mama yake Yesu, tumuombe Bikira kwa ajili &#013;\nmama zetu na kwa akina mama wote: &#8220;Salamu Maria&#8230;&#8221;.&#013;\n<\/p>\n\n<p>Salamu kubwa kwa akina mama wote, salamu kubwa!<\/p>\n\n<p>Jumapili njema kwa wote! Mlo mwema, tutaonana tena!<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>\u00abRegina Coeli\u00bb (Malkia wa Mbingu) ya Papa Fransisko kwa utume nyanjani huko Roma 7-4-2013 Fransisko Ndugu wapendwa, habari za asubuhi! Mwinjili Yohana anatuonyesha, katika Dominika hii ya 4 ya kipindi cha Pasaka, sura ya Yesu Mchungaji Mwema.Tukitafakari ukurasa huu wa Injili, tunaweza kuelewa aina ya uhusiano ambao Yesu alikuwa nao na wanafunzi wake: uhusiano unaosimama katika upole, katika upendo, katika kujuana na katika ahadi ya kipaji kisichopimika: \u201cMimi nimekuja,\u201d asema<\/p>\n<div class=\"read-more\"><a class=\"btn read-more-btn\" href=\"https:\/\/neocatechumenaleiter.org\/sw\/maneno-ya-mapapa\/fransisko\/regina-coeli-malkia-wa-mbingu-ya-papa-fransisko-kwa-utume-nyanjani-huko-roma-7-4-2013\/\">Soma zaidi<\/a><\/div>\n","protected":false},"author":2,"featured_media":0,"parent":34866,"menu_order":2,"comment_status":"closed","ping_status":"closed","template":"","meta":{"footnotes":""},"class_list":["post-48460","page","type-page","status-publish","hentry"],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/neocatechumenaleiter.org\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/pages\/48460","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/neocatechumenaleiter.org\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/pages"}],"about":[{"href":"https:\/\/neocatechumenaleiter.org\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/types\/page"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/neocatechumenaleiter.org\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/users\/2"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/neocatechumenaleiter.org\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=48460"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/neocatechumenaleiter.org\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/pages\/48460\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":48461,"href":"https:\/\/neocatechumenaleiter.org\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/pages\/48460\/revisions\/48461"}],"up":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/neocatechumenaleiter.org\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/pages\/34866"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/neocatechumenaleiter.org\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=48460"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}