{"id":37637,"date":"2024-03-15T15:50:37","date_gmt":"2024-03-15T14:50:37","guid":{"rendered":"https:\/\/neocatechumenaleiter.org\/kwa-kumbukumbu-ya-kardinali-paul-josef-cordes\/"},"modified":"2024-04-16T15:44:32","modified_gmt":"2024-04-16T14:44:32","slug":"kwa-kumbukumbu-ya-kardinali-paul-josef-cordes","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/neocatechumenaleiter.org\/sw\/kwa-kumbukumbu-ya-kardinali-paul-josef-cordes\/","title":{"rendered":"Kwa kumbukumbu ya Kardinali Paul Josef Cordes"},"content":{"rendered":"<div class=\"wp-block-image\">\n<figure class=\"aligncenter size-large\"><img loading=\"lazy\" decoding=\"async\" width=\"1024\" height=\"711\" src=\"https:\/\/neocatechumenaleiter.org\/wp-content\/uploads\/2024\/03\/camino-neocatecumenal-cardenal-cordes-juan-pablo-ii-eucaristia-1024x711.jpg\" alt=\"\" class=\"wp-image-37493\" srcset=\"https:\/\/neocatechumenaleiter.org\/wp-content\/uploads\/2024\/03\/camino-neocatecumenal-cardenal-cordes-juan-pablo-ii-eucaristia-1024x711.jpg 1024w, https:\/\/neocatechumenaleiter.org\/wp-content\/uploads\/2024\/03\/camino-neocatecumenal-cardenal-cordes-juan-pablo-ii-eucaristia-300x208.jpg 300w, https:\/\/neocatechumenaleiter.org\/wp-content\/uploads\/2024\/03\/camino-neocatecumenal-cardenal-cordes-juan-pablo-ii-eucaristia-768x533.jpg 768w, https:\/\/neocatechumenaleiter.org\/wp-content\/uploads\/2024\/03\/camino-neocatecumenal-cardenal-cordes-juan-pablo-ii-eucaristia-1536x1066.jpg 1536w, https:\/\/neocatechumenaleiter.org\/wp-content\/uploads\/2024\/03\/camino-neocatecumenal-cardenal-cordes-juan-pablo-ii-eucaristia.jpg 2040w\" sizes=\"auto, (max-width: 1024px) 100vw, 1024px\" \/><figcaption class=\"wp-element-caption\">Castelgandolfo Desemba 28, 1986. Adhimisho la Ekaristi na Baba Mtakatifu Yohane Paulo II pamoja na Mons. Cordes, Kiko Arg\u00fcello, Carmen Hern\u00e1ndez na makatekista wasafiri.<\/figcaption><\/figure><\/div>\n<div style=\"height:30px\" aria-hidden=\"true\" class=\"wp-block-spacer\"><\/div>\n\n<p><em><strong>Wenye shukrani kwa Mungu kwa huduma yake ya thamani katika Kanisa<\/strong><\/em><\/p>\n\n<p>Alfajiri ya leo (tarehe 15 Machi, 2024) Bwana amemwita Kardinali Paul Josef Cordes kwa zawadi ya uzima wa milele. Kanisa zima, na hasa Njia ya Neokatekumenato, linamshukuru sana kwa kazi aliyoifanya kwa miaka mingi ya maisha yake, akisindikiza, kupitia ushauri wake wenye busara, kuzaliwa, kukua na kuingizwa polepole ndani ya Kanisa kwa vyama na mikondo mingi sana ya kikanisa, ambayo baada ya Mtaguso imesitawi, huko akitekeleza huduma yake kama Makamu wa Raisi wa Idara ya Kipapa kwa ajili ya Walei (1980-1995).<\/p>\n\n<p>Tayari mnamo 1986 (tarehe 21 Oktoba, kupitia barua ya Katibu wa Jimbo, Kardinali Casaroli), na kwa matakwa ya Papa Yohane Paulo II, ambaye alitaka kuhamasisha uingizwaji bora wa Jumuiya za Neokatekumenato katika Kanisa, pamoja na ufafanuzi uliohitajika wa kitambulisho chake cha\u00a0 kisheria na cha kikanisa, Mons. Cordes aliagizwa kuitekeleza. Mnamo 1990, Mtakatifu Yohane Paulo II alimwandikia Mons. Cordes barua ya &#8220;<em>Ogniqualvolta<\/em>&#8220;, kama msimamizi &#8220;<em>ad personam<\/em>&#8221; (\u201ckatika nafsi yake\u201d) kwa ajili ya Utume wa Jumuiya za Neokatekumenato. Katika barua hiyo Njia ilitambuliwa &#8220;kama mwendo wa malezi ya Kikatoliki, ufaao kwa jamii na nyakati za leo&#8221;, na humo pia Papa alitamani kazi hiyo ya uinjilishaji mpya ithaminiwe na kusaidiwa na Wachungaji\u00a0.<\/p>\n\n<p>Mons. Cordes daima amekuwa na umakini na upendo wa pekee kwa waanzilishi wa Njia, Kiko Arg\u00fcello na Carmen Hern\u00e1ndez, na amewaunga mkono na kuwatia moyo katika njia yao ya ukuaji, katika vipindi vyote vya historia yao, akiwasaidia na kusindikiza hatua mbalimbali zilizoipeleka Njia ya Neokatekumenato kuidhinishwa &#8220;kama namna ya kijimbo ya uingizwaji wa kikristo na ya malezi ya kudumu ya imani&#8221; (Statuta, n. 1,2) na kutambuliwa kutoka Idara ya Mafundisho ya Imani, maandiko yote ya katekesi kama \u201cMwongozo wa Katekesi\u201d.<\/p>\n\n<p>Katika miaka hii mirefu ya historia, katika njia hii yote, Kardinali Cordes si amekuwa mtu wa karibu tu, bali pia rafiki na msaada ufaao kwa Waanzilishi na kwa Jumuiya zote za Neokatekumenato, zilizo na deni kubwa kwa kazi yake, na vile vile Wachungaji wengi aliowahimiza kusaidia na kuipatia nguvu kazi hii kwa manufaa ya Kanisa.<\/p>\n\n<p>Kwa namna ya pekee, tunakumbuka uchapishaji wa kitabu chake: \u201cKushiriki kikamilifu katika Ekaristi. \u2018Actuosa participatio\u2019 katika jumuiya ndogo\u201d katika kulinda Ekaristi iliyoadhimishwa katika jumuiya ndogo, ambayo walitetea sana Kiko na Carmen.<\/p>\n\n<p>Tunayo furaha ya kukumbuka hapa yale ambayo Papa Benedikto XVI mwenyewe alimwandikia katika barua wakati wa kuadhimisha miaka 75 ya kuzaliwa kwake:<\/p>\n\n<blockquote class=\"wp-block-quote is-layout-flow wp-block-quote-is-layout-flow\">\n<p>\u201cKwa ujasiri na ubunifu, mwanzoni mwa utendaji wako hapa Roma umefungua njia mpya za kuwaongoza vijana kwa Kristo\u2026 Umechangia pia katika kuanzisha na kukuza Siku za Vijana Duniani (SViD). Tabia yako haswa ya msukumo wako wa kichungaji imekuwa na imebakia kuwa kujitolea kwako kwa &#8220;mikondo&#8221;: Mkondo wa Wakarismatiki, Ushirika na Ukombozi (\u201cComunione e Liberazione\u201d), na Njia ya Neokatekumenato zina sababu nyingi za kuwa na shukrani kwako. Ingawa waandaaji na wapangaji wa Kanisa mwanzoni walikuwa na mashaka mengi kuhusu mikondo hii, wewe mara moja umehisi uzima uliokuwa ukijitokeza pale: nguvu ya Roho Mtakatifu inayofungua njia mpya na kwa njia isiyotabirika hulidumisha Kanisa kijana daima. Umetambua tabia ya kipentekoste ya mikondo hii na umejitolea kwa moyo mkuu kuhakikisha kwamba inakaribishwa na wachungaji wa Kanisa.&#8221;<\/p>\n<\/blockquote>\n\n<div style=\"height:30px\" aria-hidden=\"true\" class=\"wp-block-spacer\"><\/div>\n\n<p>Tunaikabidhi kwa maombi ya ndugu wote ukumbusho huu wa shukrani wa Kardinali Cordes ili wamwombe Bwana amkaribishe huyu \u201cmtumishi mwema na mwaminifu\u201d katika Ufalme wake (Mt 25,21).<\/p>\n\n<div style=\"height:30px\" aria-hidden=\"true\" class=\"wp-block-spacer\"><\/div>\n\n<h6 class=\"wp-block-heading has-text-align-right\"><strong>Kiko Arg\u00fcello, Pd. Mario Pezzi na Mar\u00eda Ascensi\u00f3n Romero<\/strong><\/h6>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Wenye shukrani kwa Mungu kwa huduma yake ya thamani katika Kanisa Alfajiri ya leo (tarehe 15 Machi, 2024) Bwana amemwita Kardinali Paul Josef Cordes kwa zawadi ya uzima wa milele. Kanisa zima, na hasa Njia ya Neokatekumenato, linamshukuru sana kwa kazi aliyoifanya kwa miaka mingi ya maisha yake, akisindikiza, kupitia ushauri wake wenye busara, kuzaliwa, kukua na kuingizwa polepole ndani ya Kanisa kwa vyama na mikondo mingi sana ya kikanisa,<\/p>\n<div class=\"read-more\"><a class=\"btn read-more-btn\" href=\"https:\/\/neocatechumenaleiter.org\/sw\/kwa-kumbukumbu-ya-kardinali-paul-josef-cordes\/\">Soma zaidi<\/a><\/div>\n","protected":false},"author":2,"featured_media":0,"comment_status":"closed","ping_status":"closed","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1343],"tags":[],"class_list":["post-37637","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-uncategorized-sw"],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/neocatechumenaleiter.org\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/37637","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/neocatechumenaleiter.org\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/neocatechumenaleiter.org\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/neocatechumenaleiter.org\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/users\/2"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/neocatechumenaleiter.org\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=37637"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/neocatechumenaleiter.org\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/37637\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":37638,"href":"https:\/\/neocatechumenaleiter.org\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/37637\/revisions\/37638"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/neocatechumenaleiter.org\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=37637"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/neocatechumenaleiter.org\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=37637"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/neocatechumenaleiter.org\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=37637"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}