Hadhira ya kutuma familia na “Missio ad gentes” 6-3-2015

Hadhira ya kutuma familia na “Missio ad gentes” 6-3-2015

Fransisko

Mji wa Vatikano – Ukumbi wa Paulo VI, 6 Machi 2015

“Ndugu wapendwa, habari za asubuhi kwenu nyote, na asanteni, asanteni sana, ninawasalimu nyote kwa moyo mkunjufu na kwanza kabisa nataka kuwaambia asante kwa kuja kukutana na Papa. Kazi ya Petro ni kuwathibitisha ndugu katika imani. Vivyo hivyo ninyi, kwa ishara hii pia mmetamani kumwomba Khalifa wa Petro kuthibitisha wito wenu, kutegemeza utume wenu, kubariki karama yenu. Na leo mimi nathibitisha wito wenu, naunga mkonoutume wenu na ninabariki katama yenu.

Na ninataka kuifanya! Ninafanya hivyo, si kwa sababu yeye amenilipa: hapana! Ninafanya kwa sababu ninataka kufanya. Mtakwenda kwa jina la Kristo ulimwenguni kote kupeleka Injili yake: Kristo na awatangulie, awasindikize na atimize wokovu ule ambao ninyi ni wabebaji wake!

Pamoja nanyi ninawasalimu Makardinali na Maaskofu wanaowasindikiza leo na ambao katika majimbo yao wanauungia mkono utume wenu. Hasa, nawasalimu waanzilishi wa Njia ya Neokatekumenato, Kiko Argüello na Carmen Hernández, pamoja na Padre Mario Pezzi: kwao vile vile ninaonyesha shukrani zangu na ninawapa moyo kwa kila kitu ambacho, kupitia Njia, wanafanya kwa manufaa ya Kanisa. Mimi nasema daima kwamba Njia ya Neokatekumenato inafanya jema kubwa kwa Kanisa.

Mkutano wetu wa leo ni wa kutuma kimisionari, kwa kutii yale ambayo Kristo ametuomba: “Nendeni ulimwenguni kote mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Anayeamini na kubatizwa, ataokolewa” (Mk 16, 15-16). Na ninafurahi sana kwamba utume wenu huu uendelezwe kupitia familia za Kikristo ambazo, zikikusanyika katika jumuiya, wako na utume wa kutoa ishara za imani zinazowavutia wanadamu kuelekea uzuri wa Injili, kulingana na maneno ya Kristo: “Mpendane kama nilivyowapenda ninyi; Katika hili wote watatambua kwamba ninyi mmekuwa wanafunzi wangu” (taz. Yn 13:34), na “Wawe kitu kimoja… ili ulimwengu upate kusadiki” (taz. Yn 17:21).

Jumuiya hizi, zinazoitwa na maaskofu, zinaundwa na mpresbiteri mmoja na familia nne au tano, zilizo na watoto wazima pia, na wanaunda “missio ad gentes”, iliyo na agizo la kuinjilisha wasio wakristo. Wasio wakristo ambao hawajawahi kusikia kuhusu Yesu Kristo na wasio Wakristo wengi ambao wamesahau Yesu Kristo alikuwa nani, Yesu Kristo alikuwa nani: “wabatizwa wasio wakristo” ambao uduniaisho, ulimwengu na mambo mengine mengi yamewafanya kusahau imani. Amsheni imani hiyo!

Kwa kuwa, hata kabla ya kwa maneno, ni kupitia ushuhuda wao wa uzima wanavyodhihirisha moyo wa ufunuo wa Kristo: kwamba Mungu anampenda mwanadamu hadi kujitoa kufa kwa ajili yake na kwamba amefufuliwa na Baba ili atupe neema ya kutoa maisha yetu kwa wengine. Ulimwengu wa leo una haja kubwa ya ujumbe huu mkuu. Ni upweke kiasi gani, mateso gani, umbali gani walio nao na Mungu katika sehemu za mbali za Ulaya na Marekani na katika miji mingi huko Asia! Jinsi gani leo mwanadamu ana haja, kwa pande zote, ya kusikia kwamba Mungu anampenda na kwamba upendo huo unawezekana! Jumuiya hizi za kikristo, kupitia ninyi, familia za kimisionari, zina jukumu la msingi la kufanya ujumbe huu uonekane. Na ujumbe huu ni upi? Kristo amefufuka, Kristo yu hai, Kristo yu kati yetu.

Ninyi mmepata nguvu ya kuacha yote na kuondoka kuelekea nchi za mbali kupitia njia ya uingizwaji wa kikristo, mnaoishi katika jumuiya ndogo, ambamo mmegundua upya hazina kubwa za Ubatizo wenu. Hii ndiyo Njia ya Neokatekumenato, zawadi ya kweli ya Upaji wa kimungu kwa Kanisa la wakati wetu, kama Watangulizi walivyosema; hasa Mtakatifu Yohane Paulo II aliposema: “Natambua Njia ya Neokatekumenato kama mwendo wa malezi ya kikatoliki inayofaa kwa jamii na kwa nyakati za leo” ( Waraka Ogniquadvolta Agosti 30, 1990: AAS 82 [1990], 1515). Njia inasimama juu ya misingi mitatu ya Kanisa, ambayo ni Neno, Liturjia na Jumuiya. Ndiyo maana ya usikivu mtiifu na endelevu wa Neno la Mungu; adhimisho la Ekaristi katika jumuiya ndogo baada ya Masifu ya kwanza ya Jumapili, kuadhimisha masifu ya asubuhi kama familia siku ya Jumapili pamoja na watoto wote, na kushiriki imani yao na ndugu wengine, huzalisha vipaji vingi ambavyo Bwana amejalia, pamoja na miito mingi mno kwa upresbiteri na maisha ya kitawa. Kuona haya yote ni faraja, kwa sababu inathibitisha kwamba Roho wa Mungu yu hai na anatenda kazi ndani ya Kanisa lake, leo pia, na kwamba anajibu mahitaji ya mtu wa kisasa.

Mara kadhaa nimesisitiza juu ya haja ya Kanisa ya kupita kutoka uchungaji wa uhifadhi tu kuelekea uchungaji wa dhati wa kimisionari (Wosia wa Kitume Evangelii gaudium, 15). Ndilo jambo muhimu zaidi tunalopaswa kufanya ikiwa hatutaki maji yatuwame katika Kanisa. Mara ngapi, Kanisani, tunaye Yesu ndani na hatumruhusu kutoka… Mara ngapi! Hili ndilo jambo muhimu zaidi la kufanya ikiwa hatutaki maji yatuwame katika Kanisa.

Kwa miaka Njia imekuwa ikifanya hizi Missio ad Gentes kati ya wasio wakristo, kwa ajili ya implantatio Ecclesiae (“kupandikiza mbegu ya Kanisa”), uwepo mpya wa Kanisa, pale ambapo Kanisa halipo au halina uwezo tena wa kuwafikia watu. “Ni furaha gani mnayotupatia kwa uwepo na utendaji wenu!” –  aliwaambia Mwenyeheri Papa Paulo VI katika hadhira yake ya kwanza nanyi (Mei 8, 1974: Mafundisho ya Papa Paulo VI, XII [1974], 407). Mimi pia ninayafanya maneno haya kuwa yangu na ninawahimiza kusonga mbele, nikiwakabidhi kwa Mtakatifu Bikira Maria, ambaye alivuvia Njia ya Neokatekumenato. Yeye anawaombea mbele ya Mungu Mwana wake.

Wapendwa, Bwana awasindikize. Nendeni, na Baraka yangu ya Kitume.