Mt. Paulo VI

Mt. Paulo VI

Wasifu

Giovanni Battista Enrico Antonio Maria Montini, alizaliwa huko Lombardy (Italia) mnamo 26 Septemba 1897.

Alipadrishwa tarehe 29 Mei 1920.

Mwaka 1954 aliteuliwa kuwa Askofu na mwaka 1958 akateuliwa kuwa Kardinali na Mtakatifu Yohane XXIII.

Tarehe 21 Juni 1963, alichaguliwa kuwa Baba Mtakatifu wa Kanisa Katoliki akichukua jina la Paulo VI.

Mwaka 1965 alianzisha Sinodi ya Maaskofu na ya Mababa wa Mtaguso.

Mtetezi wa uhai na familia kwa waraka wake wa Humanae Vitae,, aliouandika mwaka 1968. Aliuhitimisha Mtaguso wa Vatikano II.

Paulo VI alifariki huko Castel Gandolfo tarehe 6 Agosti 1978 baada ya kuwa Papa kwa miaka 15.

Alitangazwa kuwa Mwenye Heri tarehe 19 Oktoba 2014 na kutangazwa kuwa Mtakatifu tarehe 14 Oktoba 2018 na Papa Fransisko.


Hati