Hadhira ya wote 8-5-1974

Hadhira ya wote 8-5-1974

Mt. Paulo VI

Mnamo Mei 8, 1974, kama hitimisho la mkutano wa kimataifa huko Roma katika “Domus Mariae”, karibu washiriki 500, wapresbiteri na walei, waliofika kutoka nchi za Ulaya, walishiriki katika Hadhira ya Papa. Paulo VI aliwaambia maneno haya:

«Tunasalimia kundi la mapadre na walei wanaowakilisha mkondo- tazameni matunda ya mtaguso – wa Jumuiya za Neokatekumenato, waliofika hapa Roma kutoka majimbo mengi ya Italia na kutoka nchi zingine kwa ajili ya mkutano juu ya mada ya Uinjilishaji katika ulimwengu wa leo, mada ambayo itachunguzwa katika mkutano ujao wa Sinodi ya Maaskofu. Ni furaha gani na tumaini gani mnavyotupatia kwa uwepo wenu na utendaji wenu!

Tunajua kwamba katika jumuiya zenu mnajitahidi nyote kwa pamoja kuelewa na kuendeleza hazina za Ubatizo wenu, pamoja na matokeo yake kwa kuwa upande wake Kristo. Juhudi kama hiyo inawapeleka kutambua kwamba maisha ya kikristo si kitu kingine isipokuwa uwiano sawia, nguvu ya kudumu inayotokana na tukio la kukubali kukaa na Kristo na kueneza uwepo wake na utume wake duniani.

Kusudi hili, ambalo kwenu ni njia hai na halisi ya kuishi wito wa kikristo, inatafsiriwa pia katika ushuhuda wenye nguvu unaofaa kwa wengine, kichocheo kwa ajili ya ugunduzi mpya na urejesho wa thamani za kweli za kikristo, halisi, fanisi, ambazo vinginevyo zinaweza kusahaulika.

Hapana! Ninyi mnazidhirisha, mnazichipusha na kuzipatia mng’ao wa kimaadili ambao ni kielelezo halisi, kwa sababu hivyo, kwa roho hii ya kikristo, ndivyo mnavyoishi Jumuiya hii ya Neokatekumenato.

kunachukuliwa nanyi kama aina ya ukatekumeni baada ya ubatizo, ambao utaweza kufanya upya, katika jumuiya za kikristo za leo, matunda yale ya ukomavu na yenye kina ambayo katika Kanisa la kwanza yalikuwa yanafanywa katika kipindi cha maandalizi ya Ubatizo.

Ninyi mnafanya baada ya Ubatizo: kabla au baada, si muhimu. Swala ni kwamba ninyi mnatazamia uhalisi, utimilifu, uwiano sawia, unyofu wa maisha ya Kikristo. Na hii ina stahili kubwa sana, ambayo inatufariji ajabu na inatushauri na inatuvutia kuwatakia mema, sala na baraka tele kwenu na kwa wale wote wanaowaunga mkono na kwa wale ambao ninyi mnaweza kwa salamu zenu na ujumbe wenu kusalimia kutoka kwetu.

Inatufurahisha kujua kwamba mnadhamiria haya katika parokia nyingi. Tunafurahi hasa kujua kwamba katika juhudi yenu yote mnakuwa makini sana kuwategemea wachungaji wenu na ushirika na ndugu wote. Tunawahimiza kwa usikivu huu wa kikanisa, ambao daima ni dhamana ya uwepo unaojenga wa Roho.