Benedikto XVI

Benedikto XVI

Wasifu

Papa Mstaafu Benedikto XVI

Joseph Ratzinger alizaliwa huko Marktl am Inn (Ujerumani) mnamo Aprili 16, 1927.

Mnamo Juni 29, 1951, alipadrishwa huko Munich. Mnamo 1953 alipata Udaktari wa Teolojia.

Mwaka 1977 aliteuliwa kuwa Askofu Mkuu wa München na Freising na akateuliwa kuwa Kardinali mwaka 1977 na Paulo VI.

Mwaka 1981 aliteuliwa na Yohane Paulo II kuwa Mkuu wa Idara ya Mafundisho ya Imani; Raisi wa Tume ya Kipapa ya Biblia na Tume ya Kipapa ya Kiteolojia ya Kimataifa. Alikuwa Mkurugenzi wa Tume kwa ajili ya maandalizi ya Katekisimu ya Kanisa Katoliki ambayo aliwasilisha kwa Baba Mtakatifu. Mnamo Julai 3, 2015, alipokea Udaktari wa heshima “honoris causa”.

Tarehe 19 Aprili 2005, alichaguliwa kuwa Papa wa Kanisa Katoliki akichukua jina la Benedikto XVI.

Tarehe 11 Februari 2013, alijiuzulu Upapa wa Kanisa Katoliki na kuwa Papa Mstaafu.


Hati