Njia

Njia
ya Neokatekumenato

Njia ya Neokatekumenato ilizaliwa mnamo 1964 katika vibanda vya Palomeras Altas, huko Madrid (Hispania).

Kristo Pantokrator — Picha ya Kiko Argüello
Kristo Pantokrator · Kiko Argüello
Ninaitambua Njia ya Neokatekumenato kama njia ya malezi ya kikatoliki inayofaa kwa jamii na kwa nyakati za leo
Mt. Yohane Paulo II
Barua ya Ogniqualvolta
Vibanda vya Palomeras Altas, 1964
Palomeras Altas · mjini Madrid · 1964

MUHTASARI WA KITEOLOJIA-KIKATEKESI MIONGONI MWA WALIO MASKINI ZAIDI

Mazingira ya vibanda hivyo yaliundwa na watu walioharibika zaidi katika jamii: wazururaji («gypsies») na wahalifu, wengi wao wasiojua kusoma na kuandika, walalahoi, wezi, makahaba, vijana wahalifu, wahamiaji, nk. Katika mazingira haya mbegu ya Njia ya Neokatekumenato iliota. Miongoni mwa maskini na waliowekwa kando, ambao baada ya kupokea tangazo la Kristo aliyekufa na kufufuka wanaona jinsi Roho Mtakatifu anavyoinua safari ya uanzishwaji wa kikristo kwa sura ya ukatekumeni wa Kanisa la mwanzo.

Ndivyo ilivyozaliwa jumuiya ya kwanza iliyosimama katika miguu hii mitatu: Neno la Mungu-Liturujia-Jumuiya, ikiiongoza kwa ushirika wa kindugu na imani mpevu.

Neno la Mungu
Liturujia
Jumuiya

Habari za Njia ya Neokatekumenato

20.300 Jumuiya
1.392 Majimbo
6.197 Parokia
139 Mataifa
  • 116 Seminari za Redemptoris Mater (SRM)
  • 1.903 Waseminari na mashemasi 61
  • 3.263 Mapadre waliopata malezi katika SRM
  • 936 Familia katika utume, zinazoinjilisha katika Missio ad Gentes 209 katika mataifa 68.
  • 738 Zinazoimarisha na kutegemeza Njia katika imani, katika mataifa mbalimbali
  • 300 Familia zilizomo katika vikundi vya makatekista wasafiri

Imesasishwa Julai 2025:

Inabidi kufanya jumuiya za kikristo kuwa kama Familia Takatifu ya Nazareti

zinazoishi katika

unyenyekevu
urahisi
sifa
«Mwingine ni Kristo»