María Ascensión Romero
María Ascensión Romero Antón alijiunga na kikundi cha kimataifa cha Njia ya Neokatekumenato mnamo Januari 2018, baada ya Idara kwa Walei, Familia na Uhai kutoka Kiti Kitakatifu kuomba hayo, kama ilivyoelezwa katika Statuta za Njia.
Maria Ascension alizaliwa Mei 27, 1960 hukoTudela, Navarra (Hispania). Yeye ni mtoto wa tatu kati ya ndugu wanne na alisoma kwenye shule ya Shirika la Maria (hilo hilo ambapo alipata malezi Carmen Hernandez). Baadaye, alihamia Soria kusomea Ualimu na huko, akiwa na umri wa miaka 19, alifahamu Njia ya Neokatekumenato.
Alitembea miaka kadhaa katika Jumuiya ya Neokatekumenato ya Tudela hadi alipohamia Madrid kufanya kazi kama mwalimu, ambapo aliendelea na Njia katika parokia ya Mtakatifu Katarina wa Siena.
Katika SViD huko Santiago de Compostela (Hispania) pamoja na Mtakatifu Yohane Paulo II alisikia wito kwa uinjilishaji, ambao aliuthibitisha katika Mkutano wa Miito wa Zaragoza pamoja na waanzilishi wa Njia.
Mnamo 1991 alifanya utume wake wa kwanza kama msafiri katika Jimbo la Ciudad Real (Hispania). Mnamo 1992 aliondoka kuelekea utume huko USSR (Muungano wa Sovieti wa zamani), ambapo atakaa kwa miaka 25 akiinjilisha katika nchi mbalimbali: Belarus, Kazakhstan na Urusi.
Mnamo Februari 2, 2018, alitangazwa rasmi kuwa sehemu ya Kikundi cha Kimataifa cha Njia ya Neokatekumenato.