NJIA LEO

Tarehe ya Julai 19, 2016, alifariki Carmen Hernández, mwanzilishi wa Njia pamoja na Kiko Argüello, akazikwa katika Seminari ya Redemptoris Mater ya Madrid. Kwa vile kikundi cha wawajibikaji wa kimataifa kilikuwa hakijakamilika, na kwa ombi la Kiti Kitakatifu-kulingana na Statuta za Njia-, mwaka mmoja na nusu baadaye alijiunga kama sehemu ya kikundi hicho María Ascensión Romero, Mhispania, katekista msafiri kwa miaka 25 nchini Urusi.

Njia ya Neokatekumenato iko kwa huduma ya maaskofu na maparoko kama safari ya kugundua upya ubatizo na ya malezi endelevu katika imani, na inapendekezwa kwa waumini wanaotamani kufufua katika maisha yao utajiri wa uingizwaji wa Kikristo.

Njia – ambayo safari yake inafanyika katika maparokia, katika jumuiya ndogo zinazoundwa na watu wa umri na hali ya kijamii mbalimbali- hatua kwa hatua inaongoza waumini kwenye uhusiano wa kina na Yesu Kristo na kuwageuza kuwa watendaji katika Kanisa na mashahidi wa kuaminika wa Habari Njema. Ni chombo cha uanzishwaji wa kikristo kwa watu wazima wanaojiandaa kupokea ubatizo.


Habari za Njia ya Neokatekumenato

Imesasishwa mnamo Julai 2025:

Jumuiya: 20.300

Majimbo: 1.392

Parokia: 6.197

Mataifa: 139

Seminari za kimisionari za kijimbo:

Seminari za Redemptoris Mater (SRM): 116

Waseminari: 1.903 na mashemasi 61

Mapadre waliopata malezi katika SRM: 3.263

Familia za kimisionari:

Familia katika utume: 936 zinazoinjilisha katika Missio ad Gentes 209 katika mataifa 68.

Zinazoimarisha na kutegemeza Njia katika imani: 738 katika mataifa mbalimbali

Familia zilizomo katika vikundi vya makatekista wasafiri: 300