Baada ya tangazo la Kerigma jumuiya zinaibuka katika parokia, ndugu wanaoishi uingizwaji huu kwa ukristo. Hatua kwa hatua zinaanza kuonekana kati yao dalili za Imani, upendo kwa adui. Muujiza huu wa kiroho utawaita walio mbali kukutana na Yesu Kristo. Na jumuiya ya kikristo itabeba Upendo wa Mungu kwa watu wote.

“Ninyi Hamfanyi tu utume kwa sababu ya jinsi mlivyo, katika msukumo wa kugundua na kurejesha thamani za kikristo za kweli, zilizo halisi, zenye nguvu, ambazo vinginevyo zingeweza karibu kuyeyuka katika maisha ya kawaida. Hapana! Ninyi mnaziweka kwenye ushahidi, mnazifanya zitokeze, na mnazipatia mng’ao wa kimaadili ambao ni mfano halisi kwa sababu, hivyo, pamoja na roho hii ya kikristo, mnaishi jumuiya hii ya Neokatekumenato…
Ni furaha gani na tumaini gani mnavyotupatia na uwepo wenu na matendo yenu! Tunajua kwamba ndani ya jumuiya zenu mnafanya kazi pamoja ili kuelewa na kustawisha hazina za Ubatizo wenu na matokeo ninyi kuwa mali yake Kristo…
Kuishi na kukuza mwamko huu ni kile ambacho ninyi mnaita aina ya “baada ya Ubatizo” ambayo itaweza kufanya upya katika jumuiya za kikristo za leo matokeo ya ukomavu na ya kina ambayo yalitendeka katika Kanisa la mwanzo tangu kipindi cha maandalizi ya Ubatizo…
Ninyi mnafanya baadaye: kabla au baada, Naweza kusema, si muhimu. Swala ni kwamba ninyi mnatazamia uhalisi, utimilifu, uwiano sawia, unyofu wa maisha ya Kikristo».
Mt. Paulo wa Sita, Mei 8 1974
«Uzoefu na kanuni za Kanisa vimeingiza desturi takatifu ya kutoa ubatizo kwa watoto wachanga, zikiruhusu kwamba ibada ya ubatizo ifupishe kiliturjia yale maandalizi ambayo, katika vipindi vya kwanza, wakati jamii ilikuwa ya kipagani sana, yalifanyika kabla ya ubatizo, na yaliyoitwa katekumenato. Lakini katika mazingira ya kijamii ya leo namna hii inahitaji kuunganishwa na maelekezo, na uanzishwaji unaoendana na mtindo wa maisha unaofaa kwa mkristo, ukifuata ubatizo, yaani, na msaada wa kidini, na mafunzo ya vitendo kwa uaminifu wa kikristo, na kuingizwa kwa nguvu katika jumuiya ya waumini, ambayo ni Kanisa…
Tazameni hapa kuzaliwa upya kwa jina la “katekumenato”, ambayo hakika haitaki kubatilisha au kupunguza umuhimu wa mwenendo uliopo sasa wa kubatiza, bali inataka kuutekeleza kwa mbinu ya uinjilishaji wa hatua kwa hatua na wa kina, unaokumbusha na kufanya upya kwa namna fulani ile katekumenato ya nyakati nyingine. Aliyebatizwa anahitaji kuelewa, kufikiri upya, kuthamini, ili kuunga mkono utajiri usiopimika wa sakramenti iliyopokelewa.
Mt. Paulo wa Sita, Januari 12 1977