Moja ya karama kuu au matunda ya Njia ni ile ya makatekista-wasafiri. Kupitia wao imeenea katika mabara yote matano. Kikundi cha wawajibikaji wa kimataifa cha Njia kinaunda vikundi vya makatekista wasafiri – ambavyo kwa kawaida huundwa na mpresbiteri, wanandoa na mseja (mmoja wa kiume); au mpresbiteri, mseja mmoja wa kiume na mmoja wa kike–, ili kutumwa kwa mataifa kuanzisha na kuongoza utekelezaji wa Njia ya Neokatekumenato.

Makatekista wasafiri wanajibu hivi kwa maombi ya majimbo ya mbali: kikundi cha kimataifa kinawaalika ndugu wa Njia kujitolea ili kupelekwa popote duniani, na wale wanaosikia wameitwa na Mungu wanajitoa kwa hiari.
Wasafiri hupokea ombi hili ndani ya kuishi pamoja, na ndani yao kikundi cha wawajibikaji wa kimataifa cha Njia, au kingine kinachoteuliwa nao, kinathibitisha utayari na kuratibu shughuli za wasafiri, kwa mwendo wa “kubana na kuchia misuli ya moyo”, kwa kufuata mfano wa Bwana, aliyewatuma mitume wake kwenye utume, kisha akawakusanya mahali pa faragha, kusikiliza mambo ya ajabu ambayo Roho Mtakatifu alifanya nao.
Katekista msafiri anaendelea kuwa sehemu ya parokia na jumuiya yake, ambapo hurudi mara kwa mara kushiriki katika Njia ya jumuiya hiyo. Zaidi ya hayo, katekista msafiri anakubali kuishi utume wake katika hali habaishi, akiwa huru kuukatiza wakati wowote, akimfahamisha Askofu wa pale alipo na kikundi cha wawajibikaji wa Njia.