Familia katika utume

Mwaka 1985 Kiko, Carmen na Padre Mario walimwonyesha Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili mradi – uliopokelewa kwa shauku kubwa kwa upande wake – ili kuinjilisha tena Ulaya ya kaskazini kwa kutuma familia za kimisionari zinazosindikizwa na mpresbiteri. Mnamo 1986, Papa alituma familia 3 za kwanza: moja kaskazini mwa Finland, nyingine Hamburg (Ujerumani) na ya tatu Strasbourg (Ufaransa). Mnamo 1987 familia 3 za kwanza zilitumwa kwa vile vinavyoitwa “vijiji vijana ” vya Amerika ya Kusini.

Mnamo Desemba 30, 1988, Yohane Paulo II aliwasili kwa helikopta katika Senta ya Kimataifa ya Njia ya Neokatekumento huko Porto San Giorgio kutuma familia 72 popote duniani. “Kanisa Takatifu la Mungu, wewe huwezi kufanya utume wako, huwezi kutimiza utume wako duniani, ikiwa si kwa njia ya familia na utume wake.” “Familia Takatifu si kitu kingine isipokuwa hiki: familia ya kibinadamu katika utume wa kimungu. Familia katika utume, Utatu Mtakatifu katika utume. Mnapaswa kusaidia familia, mnapaswa kuilinda dhidi ya uharibifu wowote,” alisema siku hiyo Mtakatifu Yohane Paulo II.

Tangu wakati huo, karibu familia 1,800 zimetumwa na Mapapa wa mwisho kwa mabara yote matano kuinjilisha kwa ushuhuda wao wa maisha ya kikristo kwa sura ya Familia Takatifu ya Nazareti na kupitia kazi mbalimbali za kimisionari.

Ni familia ambazo, baada ya miaka mingi katika safari hii ya malezi baada ya ubatizo, ambapo nyingi zimejengwa upya, wanashukuru kwa kazi ya wokovu ambayo Mungu amefanya ndani yao. Familia hizi, wengi wao wakiwa na watoto kadhaa, wanajitolea kwenda kwenye utume wakiacha raha ya maeneo yao ya asili. Wanaenda kwenye utume popote ambapo maaskofu wanaona haja ya ushuhuda wa familia ya kikristo, wakiishi na kukita mizizi katika makanisa mahalia na kutekeleza kazi mbalimbali za uinjilishaji, wakishiriki katika upandikizaji wa jumuiya mpya za kikristo.

Katika Statuta za Njia, imeelekezwa kwamba utekelezaji wa Njia ya Neokatekumenato unaweza kusaidiwa na familia zilizo katika utume ambazo, kwa ombi la Maaskofu, zinaenda kuishi katika maeneo yaliyoacha ukristo wao au ambapo “implantatio ecclesiae” (“kanisa kupandikizwa”) inahitajika (Kifungu cha 33 [Familia katika utume], Statuta za Njia ya Neokatekumenato, Mei 11, 2008)