Jumuiya katika utume

Katika mkutano na Benedikto XVI katika Basilika la Mtakatifu Petro mnamo Januari 10 2009, kwa kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 40 ya kuzaliwa jumuiya ya kwanza ya neokatekumenato huko Roma, zilitumwa na Baba Mtakatifu Jumuiya 15 za kwanza kwa maeneo yaliyo nje kidogo ya mji wa Roma.

Jumuiya hizi zilikuwa tayari kuacha parokia yao – ambapo tayari walikuwa wamekamilisha safari ya neokatekumenato – ili kwenda kwenye utume kwa maeneo magumu ya nje ya mji kupitia mwaliko wa maparoko. Maeneo yaliyoharibiwa, yenye ukatili mwingi, madawa ya kulevya, familia zilizovunjika, wahamiaji waliowasili hivi karibuni…

Kutumwa kwa Missio ad Gentes kutoka Basilika la Mt. Petro

Kiko, akitambulisha utume huu mpya, alisema kwamba “Njia inaisha kwa kutangaza Injili ulimwenguni kote. “Moja ya mambo mapya zaidi ni kwamba jumuiya nzima inaenda kwenye utume. Siyo baadhi ya ndugu, jumuiya nzima inaenda. Ni neema kubwa sana na ni kitu cha ajabu kwamba Mungu awatume kwa utume huu. Ni ajabu kuweza kuondoka, kwamba Bwana akupatie utume; kufa katika utume, kuzeeka katika utume.”

Kwa namna sawia, Papa Fransisko katika barua yake ya Evangelii Gaudium anazungumza juu ya Kanisa “linalotoka nje” na kuelezea hitaji la kuinjilisha maeneo ya “nje”, kijiografia na kimaisha: “

Pia jimbo la Madrid, ambapo Njia ilizaliwa na ipo katika parokia 45 zenye jumuiya 221, yako maang’amuzi haya. Mwaka 2011, Askofu Mkuu wa Madrid wakati huo, Kardinali Rouco Varela alituma jumuiya 10 za kwanza kwenye utume.

Askofu Mkuu wa sasa wa mji mkuu wa Hispania, Kardinali Carlos Osoro Sierra, katika mkutano wa Machi 22, 2015, alituma jumuiya 8 mpya. Huko Madrid, kuna jumla ya jumuiya 18 katika utume.

Tarehe 5 Mei 2018, Papa Fransisko, katika kuadhimisha miaka 50 ya kuzaliwa kwa jumuiya ya kwanza ya Njia huko Roma, katika mkutano mkubwa huko Tor Vergata (Roma) alituma jumuiya 25 kwenye utume kwa parokia mbalimbali za Roma ili kutegemeza na kuimarisha maisha ya kikristo ya jumuiya za parokia zenye magumu zaidi.

Leo, katika ‘nendeni’ hii ya Yesu, yamo mazingira na changamoto mpya za utume wa kuinjilisha wa Kanisa, na sote tumeitwa kwa “mtoko” huu mpya wa kimisionari. Kila mkristo na kila jumuiya itapambanua ipi ndiyo njia ambayo Bwana anaomba kwake, lakini sote tunaalikwa kukubali wito huu: kutoka katika raha yako na kuthubutu kuyafikia maeneo yote ya mbali yanayohitaji nuru ya Injili”.