Hadhira binafsi kwa waanzilishi wa Njia ya Neokatekumenato 19-11-2005

Hadhira binafsi kwa waanzilishi wa Njia ya Neokatekumenato 19-11-2005

Benedikto XVI

Mji wa Vatikano, tarehe 19 Novemba 2005

Tarehe 19 Novemba 2005, Baba Mtakatifu Benedikto XVI, aliwapokea katika Hadhira binafsi, kwa mara ya kwanza, waanzilishi wa Njia ya Neokatekumenato.

Kiko ameeleza mkutano huo kwa maneno haya:

“Umekuwa mkutano mzuri ajabu. Tulikuwa tumemwomba Papa Hadhira, tukijua kwamba ilikuwa vigumu sana na hata hivyo ametujalia. Mei iliyopita tulikuwa na kuishi pamoja na familia na tulituma 200. Tumemwuliza Papa Benedikto XVI ikiwa angeweza, kama alivyofanya Yohane Paulo II alipotuma familia zaidi ya 400 duniani kote, kuwapatia msalaba kwa familia hizi mpya na kupiga picha pamoja nao ili waonyeshe, popote waendapo, kwamba ni wakatoliki, kwa sababu wataenda kwenye mazingira magumu sana ya Amerika na kaskazini mwa Ulaya. Wametufahamisha kwamba tarehe 12 Januari Papa atafurahi kuweza kuzituma familia hizi 200 duniani kote. Ni mkutano muhimu sana! Itakuwa mara ya kwanza ambapo Papa Benedikto XVI atasema neno kuhusu Njia ya Neokatekumenato mbele ya Kanisa zima. Wote wanasubiri”.

Hadhira binafsi tuliyoishi tarehe 19 Novemba ilikuwa nzuri mno: niliongea kidogo kuhusu mpango wa uinjilishaji ambao tulikuwa tumewasilisha kwa Yohane Paulo II, na “implantatio Ecclesiae” (Kanisa kupandikiziwa) kupitia familia kwenye utume, kidogo kama alivyofanya Mtakatifu Benedikto; nimemwonyesha Papa ramani inayoonyesha seminari 27 za Ulaya na mahali ambapo familia ziko kwenye utume… Basi, zilipokuwa zimesalia dakika 5 kabla ya mwisho wa Hadhira, Papa alisema: “Vizuri sana, sasa tuzungumze kuhusu liturjia. Jana nilizungumza na Kadinali Arinze na tumekubaliana kuhusu baadhi ya mambo.” Ametuambia kwamba tunaweza kufanya utangulizi mfupi kwa masomo, miangwi michache kwa neno, 3 au 4, ambayo bila shaka haitachukua nafasi ya homilia. Amani inabaki pale tunapoifanya, na kuhusu komunyo kwa maumbo yote mawili tunaweza kuendelea kuifanya kama vile tumekuwa mpaka sasa, baadaye tutaona.