Uchaguzi wa Papa Leo XIV
Njia ya Neokatekumenato imepokea habari za kuchaguliwa kwa Kardinali Robert Prevost kuwa Khalifa wa Petro kwa furaha kubwa. Maneno yake ya kwanza yametujaza furaha, akimweka Kristo Mfufuka kama kiini cha yote, ambaye anatupatia amani yake, pamoja na uinjilishaji unaozaliwa kutoka katika moyo wa kimisionari. Kumekuwa na mwangwi wa pekee katika mioyo ya ndugu wote wa Njia—na hasa ule wa kwangu— kutokana na kwamba uchaguzi huu ulifanyika siku ya Bikira Maria