Mpito kwa Baba wa Benedict XVI – Ujumbe kutoka Kiko Argüello

UJUMBE WA KIKO KWA JUMUIYA ZA NEOKATEKUMENATO Madrid tarehe 31 Desemba 2022 Kumbukumbu ya Mtakatifu Silvester, Papa Ndugu wapendwa: Tumepokea hivi punde habari za kwenda kwa Baba kwa Papa Mstaafu Benedict XVI. Nakwakumbusha kwamba, tangu alipokuwa Profesa, na baadaye akiwa Mkuu wa Idara ya Mafundisho ya Imani, na kisha akiwa Papa, tumekuwa daima na shukrani ya pekee na upendo kwake; baada ya Papa Mtakatifu Paulo VI na Papa Mtakatifu Yohane

Sala kwa ajili ya Papa Benedict XVI

Madrid, 29 Desemba 2022 Ndugu wapendwa: Papa Fransisko, kwenye hadhira yake kuu Jumatano iliyopita, ameliomba Kanisa zima la Ulimwengu kuinua maombi kwa ajili ya Papa Mstaafu Benedict XVI, ambaye afya yake imedhoofika sana katika siku za hivi karibuni. Sisi ndugu wa Njia ya Neokatekumenato tunajiunga na ombi hili. Ni kiasi gani tunachopaswa kumshukuru Papa Benedict kwa upendo wake kwa ajili ya Njia, uliodhihirishwa katika matukio mengi mbali mbali! Tusali pamoja

Hija Fuentes de Carbonero el Mayor (Segovia – Hispania)

Kanisa la Fuentes de Carbonero Mahali pa kuhiji na kuadhimisha, ushuhuda wa historia ambayo Mungu hufanya pamoja nasi. «Nilishangaa sana kwamba wakati nyumba zote katika kijiji hicho ziliharibika, kitu pekee kilichobaki kikisimama katika kijiji hicho kilichotelekezwa kilikuwa kanisa, na kanisa ambalo limejaa maskini.Hapa tulisherehekea Mkesha wa Pasaka na ndugu wa vibandani na wale wa jumuiya ya kwanza ya Madrid. Hatukuwa na umeme; Tulijiangazia na nuru ya mshumaa mkubwa wa zamani

Ufunguzi wa Mchakato wa Kutangazwa Mwenye Heri kwa Mtumishi wa Mungu Carmen Hernández

“Yesu wangu, nipeleke kwenye utakatifu wako”; “Wewe unaniongoza kwenye utakatifu” (“Kitabu cha kumbukumbu 1979-1981”, na. 85; na.199) Tarehe Desemba 4, 2022, “Tukio” lenye nguvu na maana maalum kwa Kanisa zima lilitukia huko Madrid: ufunguzi wa hatua ya kijimbo ya Kutangazwa Mwenye Heri na Kutangazwa Mtakatifu kwa Carmen Hernández Barrera, mwanzilishi mwenza, pamoja na Kiko Argüello, wa njia hiyo ya uanzishwaji wa kikristo inayoitwa Njia ya Neokatekumenato. Ufunguzi wa mchakato Katika

Ufunguzi wa Mchakato wa Kutangazwa Mwenye Heri na Kutangazwa Mtakatifu wa Carmen Hernández

Mubashara Kutoka Madrid (Hispania), jumapili tarehe 4 Desemba, 2022,  saa 2 usiku, East Africa Time (GMT +03:00)  Jimbo Kuu la Madrid Kituo cha michezo cha Chuo Kikuu cha Francisco Vitoria. Anaongoza ibada Kard. Carlos Osoro, Askofu Mkuu wa Madrid. Waanzilishi wa Mchakato: Kiko Argüello, P. Mario Pezzi, Ascensión Romero, Taasisi za “Familia ya Nazareti” za Roma na Madrid. Mwombaji: Carlos Metola.

Siku ya Vijana Duniani – SViD Lisbon 2023

Ndugu wapendwa, Kutoka Ureno tunawapatia taarifa kuhusu Siku ya Vijana Duniani (SViD) ijayo, huko Lisbon 2023. Tarehe rasmi za siku hizo ni kuanzia tarehe 1 hadi 6 Agosti 2023. Mkesha na Baba Mtakatifu utakuwa Jumamosi tarehe 5 na Ekaristi ya mwisho Jumapili tarehe 6. Tovuti rasmi (kwa kiingereza) ya SViD ni: Kusajili kwa Mkutano huo, kwa zake mbalimbali, kutafunguliwa mwishoni mwa Oktoba. Ni muhimu sana usajili rasmi, kwa sababu kadiri