Siku ya Ijumaa, tarehe 5 Mei 2023, katika Idara ya Michakato ya Watakatifu ya Vatikano, kumekuwa na tukio la Ufunguzi wa masanduku ya Maandiko ya mchakato wa kijimbo wa kutangazwa Mwenye heri na Mtakatifu kwa Marta Obregón kwa njia ya kifo cha kishahidi.

Bi. Cristiana Marinelli, mwombaji wa awamu ya kirumi ya Mchakato, Bw. Carlos Metola, mwakilishi wa upande wa kitendaji wa Mchakato, Bw. Saturnino López, mwombaji wa awamu ya kijimbo na ofisa wa Idara ya Michakato ya  Watakatifu ya Vatikano.
Waombaji wa Mchakato wa Marta Obregón

Limekuwa tukio rahisi lakini lenye adhama, la kupendeza na lenye hisia kubwa. Hatua hii inaashiria endeleo la utafiti wa kina unaotekelezwa katika awamu hii ya pili. Walihudhuria mtangazaji mpya wa awamu ya Roma, Bi. Cristiana Marinelli, mpresbiteri mwombaji wa awamu ya kijimbo, Padre Saturnino López, na Bw. Carlos Metola, mwakilishi wa waombaji wa Mchakato (Njia ya Neokatekumenato).

Marta Obregón alikuwa msichana mwenye furaha, mchangamfu sana, ambaye alikuwa ndani ya jumuiya ya neokatekumenato katika parokia ya Mt. Martín de Porres huko Burgos, Hispania. Alikuwa mmojawapo wa waimbaji wa jumuiya yake.

Alipokuwa na umri wa miaka 22 na alikuwa akisoma mwaka wa mwisho wa shahada yake ya Uandishi wa Habari, “alisimama” kwa ajili ya unijilishaji katika Kuishi Pamoja ya Mwanzo wa Mwaka, yaani, alijitolea kutumwa sehemu yoyote ya dunia kama mmisionari msafiri. Miezi hiyo ya mwisho ya maisha yake alitafuta kufanya mapenzi ya Mungu, na katika “miangwi” yake na “sala” zake katika maadhimisho ya jumuiya yake alirudia mara nyingi: “Bwana, na itendeke”.

Usiku wa Januari 21, 1992, alifikiwa mlangoni mwa nyumba yake, akatekwa nyara na kupelekwa kikatili kwenye uwanja wazi, nje ya jiji, ili kubakwa na muuaji wake. Marta alitetea fadhila ya usafi kwa namna ya kishujaa, hadi kifo. Alipata majeraha 14 ya kuchomwa na kisu (sawa na yale aliyoyapata mtakatifu Maria Goretti), mojawapo lilimchoma moja kwa moja moyoni, na alikufa Januari 21 (sikukuu ya kiliturjia ya Mtakatifu Anyesi, bikira na shahidi).

Katika parokia yake na katika jiji lote la Burgos, na pia katika mahali pengi huko Hispania na ulimwenguni kote, umewasili “umaarufu wa utakatifu na kifo cha kishahidi” wa msichana huyu mwenye kupenda kuwasiliana na mchangamfu, ambaye alizungumza waziwazi kuhusu utendaji wa Mungu. Katika maandishi ya Marta muda mfupi kabla ya kufa aliandika maneno haya ya kina kuhusu maisha yake:

Maandiko ya mchakato wa kijimbo wa Kutangazwa Mwenye heri na Mtakatifu

“Ninaanza kutambua kitu kimoja: kwamba napaswa kuishi wakati huu, sasa, na ndipo tu nitaweza kugundua yale ya kabla, ambacho ni MAPENZI yako, na daima KILICHO BORA ZAIDI kwangu juu ya yote, juu ya YOTE ambayo ulimwengu hunipa. ”

Tunamshukuru Mungu kwa hatua hii mpya ambayo Kanisa linachukua na Marta Obregón na ambayo inazidisha tumaini letu. Katika ulimwengu ambamo uchafu (kwa tamaa za mwili) unakua na kuharibu kazi ya Muumbaji, mfano wa Marta Obregón, kwa utetezi wa kishujaa wa usafi, unakuwa nuru kwa vijana na wabalehe wa karne ya 21 ambao, wakishambuliwa na itikadi ya jinsia na kupotezwa maana kwa tendo la ngono, wengi hawafahamu heshima ya mwili na thamani ya ubikira, wakisababishiwa mateso mengi. Tumwombe Bwana ili mchakato huu uendelee kwa bidii na uwe mfano na faraja kwa vijana wa Njia ya Neokatekumenato na Kanisa zima.

Share: