Uteuzi wa Wajumbe wa Idara ya Uinjilishaji. Kitengo cha maswala ya msingi ya uinjilishaji duniani.
Baba Mtakatifu Fransisko anawakaribisha kikundi cha kimataifa cha Njia tarehe 20 Septemba 2019
Papa Fransisko anawakaribisha Kikundi cha Kimataifa cha Njia ya Neokatekumenato tarehe 20 Septemba 2019

Baba Mtakatifu, Papa Fransisko ameteua leo tarehe 25 Aprili 2023 Wajumbe wa Idara ya Uinjilishaji, Kitengo cha Maswali ya Msingi ya Uinjilishaji Duniani, kwa muhula wa miaka 5. Miongoni mwao, pamoja na makardinali kumi kutoka sehemu mbalimbali za dunia, maaskofu wakuu wanne na maaskofu, mtawa wa kike na walei wengine watatu, ameteuliwa Dada María Ascensión Romero Antón, ambaye ni wa Kikundi cha Kimataifa cha Wajibikaji wa Njia ya Neokatekumenato.

María Ascensión Romero ameonyesha shukrani zake kwa Baba Mtakatifu kwa imani aliyoweka kwake na kwa Njia nzima ya Neokatekumenato kupitia uteuzi huu, na amemhakikishia sala yake na ushirikiano wake kamili katika utume huu. Pia anawaomba ndugu wa Njia ya Neokatekumenato wamsaidie yeye, pamoja na Idara nzima ya Uinjilishaji, kupitia sala zao.

Share: