Ufunguzi wa Mchakato wa Kutangazwa Mwenye Heri kwa Mtumishi wa Mungu Carmen Hernández

“Yesu wangu, nipeleke kwenye utakatifu wako”; “Wewe unaniongoza kwenye utakatifu” (“Kitabu cha kumbukumbu 1979-1981”, na. 85; na.199) Tarehe Desemba 4, 2022, “Tukio” lenye nguvu na maana maalum kwa Kanisa zima lilitukia huko Madrid: ufunguzi wa hatua ya kijimbo ya Kutangazwa Mwenye Heri na Kutangazwa Mtakatifu kwa Carmen Hernández Barrera, mwanzilishi mwenza, pamoja na Kiko Argüello, wa njia hiyo ya uanzishwaji wa kikristo inayoitwa Njia ya Neokatekumenato. Ufunguzi wa mchakato Katika

Ufunguzi wa Mchakato wa Kutangazwa Mwenye Heri na Kutangazwa Mtakatifu wa Carmen Hernández

Mubashara Kutoka Madrid (Hispania), jumapili tarehe 4 Desemba, 2022,  saa 2 usiku, East Africa Time (GMT +03:00)  Jimbo Kuu la Madrid Kituo cha michezo cha Chuo Kikuu cha Francisco Vitoria. Anaongoza ibada Kard. Carlos Osoro, Askofu Mkuu wa Madrid. Waanzilishi wa Mchakato: Kiko Argüello, P. Mario Pezzi, Ascensión Romero, Taasisi za “Familia ya Nazareti” za Roma na Madrid. Mwombaji: Carlos Metola.