Papa anampokea Kiko Argüello, mwanzilishi wa Njia ya Neokatekumenato

Asubuhi ya leo, Jumamosi, tarehe 27 Januari 2024, Papa Fransisko aliwapokea katika hadhira binafsi Kikundi cha Kimataifa cha wajibikaji wa Njia ya Neokatekumenato: mwanzilishi Kiko Argüello, Padre Mario Pezzi na Ascensión Romero. Katika hadhira hiyo, Kikundi walimjulisha Baba Mtakatifu kuhusu Kuishi Pamoja ya Kiulimwengu, ambayo imehitimishwa hivi punde, ikiwa na zaidi ya makatekista wasafiri 1,000, wanaowajibika kwa mataifa 136 ambapo Njia ya Neokatekumenato ipo, na Magombera wa Seminari za Kimisionari

Papa kwa familia za Njia ya Neokatekumenato zilizotumwa katika utume

Kiko Argüello Baba Mpendwa: Asante kwa uwepo wako, asante kwa kukubali kutuma familia hizi katika utume. Tunawasalimu Kardinali Kevin Farrell, Maaskofu wakuu na Maaskofu waliopo, na pia washiriki kutoka Idara ya Walei, Familia na Uhai, ambao wamekubali kushiriki tukio hili pamoja nasi. Baba Mtakatifu, kabla hatujaanza, tunataka kukushirikisha habari ambayo tunajua itakufurahisha: Jimbo kuu la Madrid limetufahamisha kwamba mchakato wa kutangazwa kuwa mwenye heri na wa kuwa mtakatifu wa Carmen

Papa anatuma kwenye ututme familia 430 za Njia ya Neokatekumenato

Leo tarehe 27 Juni 2022, wakati wa kuhitimisha Mkutano wa Kumi wa Familia Duniani, Baba Mtakatifu Fransisko, aliyekaribishwa kwa furaha katika Ukumbi wa Paulo wa Sita kwa wimbo wa Bikira Maria, alituma Familia 430 za Njia ya Neokatekumenato, pamoja na watoto wao, hadi sehemu zilizopoteza zaidi Ukristo wao ulimwenguni ili kuonyesha kwa maisha yao ushuhuda wa upendo wa Mungu kwa walio mbali zaidi. Pamoja na Familia hizi, walikuwepo Kikundi cha