Papa kwa familia za Njia ya Neokatekumenato zilizotumwa katika utume

Kiko Argüello Baba Mpendwa: Asante kwa uwepo wako, asante kwa kukubali kutuma familia hizi katika utume. Tunawasalimu Kardinali Kevin Farrell, Maaskofu wakuu na Maaskofu waliopo, na pia washiriki kutoka Idara ya Walei, Familia na Uhai, ambao wamekubali kushiriki tukio hili pamoja nasi. Baba Mtakatifu, kabla hatujaanza, tunataka kukushirikisha habari ambayo tunajua itakufurahisha: Jimbo kuu la Madrid limetufahamisha kwamba mchakato wa kutangazwa kuwa mwenye heri na wa kuwa mtakatifu wa Carmen