Kwa kumbukumbu ya Kardinali Paul Josef Cordes

Wenye shukrani kwa Mungu kwa huduma yake ya thamani katika Kanisa Alfajiri ya leo (tarehe 15 Machi, 2024) Bwana amemwita Kardinali Paul Josef Cordes kwa zawadi ya uzima wa milele. Kanisa zima, na hasa Njia ya Neokatekumenato, linamshukuru sana kwa kazi aliyoifanya kwa miaka mingi ya maisha yake, akisindikiza, kupitia ushauri wake wenye busara, kuzaliwa, kukua na kuingizwa polepole ndani ya Kanisa kwa vyama na mikondo mingi sana ya kikanisa,

Papa anampokea Kiko Argüello, mwanzilishi wa Njia ya Neokatekumenato

Asubuhi ya leo, Jumamosi, tarehe 27 Januari 2024, Papa Fransisko aliwapokea katika hadhira binafsi Kikundi cha Kimataifa cha wajibikaji wa Njia ya Neokatekumenato: mwanzilishi Kiko Argüello, Padre Mario Pezzi na Ascensión Romero. Katika hadhira hiyo, Kikundi walimjulisha Baba Mtakatifu kuhusu Kuishi Pamoja ya Kiulimwengu, ambayo imehitimishwa hivi punde, ikiwa na zaidi ya makatekista wasafiri 1,000, wanaowajibika kwa mataifa 136 ambapo Njia ya Neokatekumenato ipo, na Magombera wa Seminari za Kimisionari

“MASIYA” ya Kiko Argüello

Trieste, Italia – 19 Novemba 2023 – saa mbili usiku. Shairi la kisinfonia linalotolewa kwa ajili ya mashahidi. Jumapili tarehe 19 Novemba, saa mbili usiku, katika Teatro Verdi huko Trieste (Italia) onyesho mashuhuri la kwanza duniani litafanyika. Kipengele cha kwanza ni simfonia yenyewe ya “Masiya”, ambayo inaundwa na sehemu tatu: “Akeda”, “Binti za Yerusalemu” na “Masiya, simba kwa kushinda”. Katika hizi tatu kuna hewa ya kisimfonia ambapo kinanda kinachukua sehemu

Wimbo wa matumaini

Habari za hivi punde: Takwimu rasmi kutoka kwa ulinzi wa raia na polisi wa Lisbon zinathibitisha mahudhuria¡o ya zaidi ya watu 100,000 kwenye mkutano wa miito VIJANA WA NJIA YA NEOKATEKUMENATO WAJAZA MIJI YA ULAYA KWA NYIMBO. Toleo la 37 la Siku ya Vijana Duniani (Lisbon, Agosti 1-6, 2023) lilikuwa na dakika ya mwisho ya furaha ya ajabu katika mkutano wa Vijana zaidi ya elfu sabini na tano wa Njia

Maelfu ya vijana watashiriki katika mkutano wa miito wa Njia ya Neokatekumenato huko Lisbon ndani ya mfumo wa SViD (Siku ya Vijana Duniani).

Jumatatu ijayo, Agosti 7, watakutana kutoka mabara matano pamoja na makardinali na maaskofu mbalimbali Njia ya Neokatekumenato, kama ilivyo desturi katika Siku za Vijana Duniani, itaadhimisha Mkutano wa Miito kwa sababu ya SViD huko Lisbon 2023. Itakuwa Jumatatu ijayo, Agosti 7 4:30 p.m (GMT +1) kwenye Paseo Marítimo ya Algés. Watashiriki zaidi ya vijana 75,000 kutoka sehemu mbalimbali za dunia, watakaokuwa wamemsindikiza Baba Mtakatifu Fransisko katika wiki ya maadhimisho ya