Jumatatu ijayo, Agosti 7, watakutana kutoka mabara matano pamoja na makardinali na maaskofu mbalimbali
SViD Cologne, Ujerumani 2005
Carmen Hernández na Kiko Argüello SViD Ujerumani 2005

Njia ya Neokatekumenato, kama ilivyo desturi katika Siku za Vijana Duniani, itaadhimisha Mkutano wa Miito kwa sababu ya SViD huko Lisbon 2023. Itakuwa Jumatatu ijayo, Agosti 7 4:30 p.m (GMT +1) kwenye Paseo Marítimo ya Algés. Watashiriki zaidi ya vijana 75,000 kutoka sehemu mbalimbali za dunia, watakaokuwa wamemsindikiza Baba Mtakatifu Fransisko katika wiki ya maadhimisho ya SViD.

Mkutano wa Njia utaongozwa na kikundi cha wawajibikaji cha kimataifa, kilichoundwa na mwanzilishi wake, Kiko Argüello, Padre Mario Pezzi na María Ascensión Romero.

Mkutano utaongozwa na Patriaki wa Lisbon, Kardinali Manuel Clemente. Ndani yake Kerigma itahubiriwa, Habari Njema ya kifo na ufufuko wa Kristo, na miito itaitishwa kwa wale vijana ambao wanahisi wameitwa na Bwana kwa maisha ya kitawa, utume wa kisafiri au upresbiteri.

Kwa miaka minne, tangu SViD huko Panama, vijana wa Njia wamekuwa wakijiandaa kuhiji huko Lisbon. Siku za kabla ya kuwasili kwa Baba Mtakatifu na mpito wake katika nchi na miji mbalimbali, watainjilisha wakitoa ushuhuda wa mkutano wao na Bwana. Kama vile Papa Fransisko anavyorudia mara nyingi, akichukua maneno kutoka Benedict XVI, “Kanisa halikui kwa kushawishi watu, bali kwa kuwavutia.”

Siku hizi kabla ya SViD huko Lisbon na ya Mkutano wa Miito zimeingiliana na kumbukumbu ya miaka saba ya kifo cha Carmen Hernández, mwanzilishi mwenza wa Njia ya Neokatekumenato pamoja na Kiko Arguello. Tarehe 19 Julai, siku ya kumbukumbu hiyo, maelfu ya vijana hawa waliadhimisha Ekaristi kwa ajili ya roho ya Carmen katika parokia mbalimbali duniani kote, wakimwomba Bwana aharakishe Mchakato wake wa Kutangazwa Mwenye heri na Mtakatifu.

Carmen Hernández

Vijana kutoka mataifa mengi, wanaopitia Madrid wakielekea Lisbon, wanazuru kaburi la Carmen Hernández. Seminari ya Redemptoris Mater ya Madrid tayari inaonjeshwa furaha ya SViD kupitia uwepo wa vijana wengi hivi wanaomshukuru Bwana kwa zawadi ya maisha ya Carmen na upendo wake kwa utume na kwa Kanisa.

Share: