Hatua mpya katika awamu ya Roma ya Mchakato wa Kutangazwa Mwenye heri kwa Marta Obregón

Siku ya Ijumaa, tarehe 5 Mei 2023, katika Idara ya Michakato ya Watakatifu ya Vatikano, kumekuwa na tukio la Ufunguzi wa masanduku ya Maandiko ya mchakato wa kijimbo wa kutangazwa Mwenye heri na Mtakatifu kwa Marta Obregón kwa njia ya kifo cha kishahidi. Limekuwa tukio rahisi lakini lenye adhama, la kupendeza na lenye hisia kubwa. Hatua hii inaashiria endeleo la utafiti wa kina unaotekelezwa katika awamu hii ya pili. Walihudhuria