
Njia ya Neokatekumenato ni safari ya malezi ya kikatoliki inayotekelezwa katika majimbo kupitia huduma za bure (taz. Kifungu cha 4 cha Statuta za Njia ya Neokatekumenato), iliyoidhinishwa na Kiti Kitakatifu.
Mikusanyiko ya maadhimisho ya jumuiya hutumia nyenzo mbalimbali (nyimbo, ishara za kiliturujia na michoro), ambazo ni matunda ya ubunifu wa Kiko Argüello na Carmen Hernández, ambao, bila kutafuta faida, wamezifanya zipatikane bila gharama yoyote kwa ndugu wa jumuiya na parokia kwa ajili ya matumizi ya kiliturujia.
Katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na usambaaji usiodhibitiwa wa nyenzo hizi katika mitandao ya kijamii, imepasa kusajili kazi za Kiko ili kuhakikisha matumizi yao bure na ndugu wa jumuiya, pamoja na kutetea uhalisi wao na madhumuni ya asili. Kwa hakika, baadhi wamesambaza nyenzo hizi isivyofaa, wakiyabadilisha au wakizuia matumizi yake huru na bila malipo inavyofaa.
Kwa lengo hilo, umeombwa uundaji wa taasisi ya kijimbo iitwayo “Obra Artística Kiko Argüello”, yenye jukumu la kuhifadhi uhalisi, madhumuni, na matumizi ya kazi hizo.
Nyimbo za kiliturujia za Kiko zimesajiliwa na SIAE (Jumuiya ya Italia ya Waandishi na Wachapishaji).
Inafaa pia kufahamu kwamba Waanzilishi wa Njia siku zote wametamani kwamba katekesi za zifundishwe ana kwa ana, kwa kutumia njia ya mapokeo ya mdomo, wala yasishirikishwe kwenye mitandao ya kijamii, kwa kuwa kiini chao kinapatikana katika adhimisho la kikatekesi na la kiliturujia.
NYONGEZA
Kulingana na Statuta, zilizoidhinishwa rasmi na Kanisa, Njia ya Neokatekumenato ni mojawapo ya taratibu za kijimbo za unazishwaji wa Kikristo, chini ya mamlaka ya Askofu mahalia na inaongozwa na makatekista walioteuliwa kwa kushirikiana naye. Si chama wala mkondo. Kwa hiyo, washiriki wake hawana kadi za uanachama, na hivyo hakuna mtu anayeweza kuandikishwa wala kufukuzwa. AIdha, hakuna mapadre “wa Njia,” bali ni mapadre wa kijimbo waliopata malezi katika seminari ya kijimbo ya kimisionari, iliyosimikwa na Askofu, na kwa hivyo, katika utii kwake. Makatekista, ambao huangalia ustawi wa ndugu wa jumuiya hizi na ushirika miongoni mwa wote, wanaweza kuingilia kati wakati kuna hatari ya mgawanyiko au kupotea kwa ushirika wa kikanisa, na kumwomba ndugu huyo achukue muda wa kutafakari.