Njia ya Neokatekumenato inaadhimisha kumbukumbu ya miaka 50 huko Oviedo (Hispania) kwa uwepo wa Kiko Argüello na Askofu Mkuu Mha. Jesús Sanz Montes.
Tamasha huko Oviedo

Ili kuadhimisha miaka 50 ya Njia ya Neokatekumenato huko mkoani Asturias, katika mji wa Oviedo, Askofu Mkuu Mons. Jesús Sanz Montes aliongoza Mkesha wa Sherehe ya Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili pamoja na jumuiya za Neokatekumenato za mji huo mkuu Mkoa wa Asturias.

Siku ya Jumatatu, Desemba 8, Kiko Argüello aliwasilisha kazi yake ya kisimfonia katika Ukumbi wa Mwana Mfalme Felipe huko Oviedo. Kabla ya tamasha kuanza, Askofu Mkuu wa jimno, Mha. Jesús Sanz, alifungua tukio hilo kwa sala mbele ya wahudhuriaji 1,500, na pamoja nao zaidi ya watu 24,000 waliounganishwa mtandaoni. Miongoni mwa waliohudhuria walikuwa kutoka jumuiya za Njia ya Neokatekumenato kutoka Kaskazini Magharibi mwa Hispania na Seminari za Redemptoris Mater za Oviedo, León, Lugo, Orense, Burgos, Vitoria, Murcia, na Bayonne.

“Kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Tunakushukuru, Bwana, kwa kutkutanisha huku ili kukumbuka historia iliyoanza hapa miaka 50 iliyopita na ambayo siku baada ya siku ndugu wanaendelea kuandika. Maisha ni simfonia isiyokamilika; wewe unaweka herufi ya historia zetu, nasi kwa unyenyekevu tunaweka muziki wa nota zetu. Pamoja nawe tunaunda uzuri unaoweza kuongoa na kufungua mioyo ya wale unaotutuma kwao kuwatangazia Kerygma inayowaokoa. Chini ya ulinzi wa Mama yetu, Bikira Mkingiwa dhambi ya asili, na wa Watakatifu wetu wote, tunakutolea tukio hili kama heshima ya shukrani kwa ajili ya historia inayoendelea ya Njia ya Neokatekumenato hapa Asturias. Atukuzwe Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu”.

Mons. Jesús Sanz Montes

Kiko Argüello aliingilia akisema:

“Nimefurahi sana kusherehekea tamasha katika sikukuu hii, kwa sababu Njia ya Neokatekumenato ilivuviwa na Mtakatifu Bikira Maria hasa katika siku ya Kukingiwa Dhamni ya Asili”.

Katika kuwasilisha kazi yake ya kwanza ya kisimfonia, “Mateso ya Wasio na Hatia”, Kiko alielezea jinsi ambavyo ameguswa daima na sura ya Mtumishi wa Yahweh iliyotangazwa na Isaya, huko akihusianisha picha hii na Leso Takatifu ya Oviedo na Sanda Takatifu la Turin:

“Mtu aliyejaa huzuni, ambaye majeraha yake yametuletea amani. Uso wake nimeuchora mara kadhaa, nikifuata mfano wa Sanda la Turin. Nilishangazwa kufahamu kwamba utafiti wa hivi karibuni unamtambulisha mtu kwenye Sanda la Turin na yule wa anayeonekana katika Leso Takatifu lililohifadhiwa zaidi ya miaka 1,000 katika Kathedrali ya Oviedo. Mapokeo ya Kanisa yanasema kwamba kitambaa hiki kidogo cha kitani ndicho Leso Takatifu iliyofunika kichwa cha Kristo baada ya kifo chake. Uchunguzi wa hivi karibuni unathibitisha kwamba kilifunika kichwa cha mtu aliyesulubiwa, aliyevikwa taji la miiba na mwenye majeraha mengi”.

Baada ya Simfonia kupigwa, Kiko alitambulisha Shairi la Kisimfonia “Masiya”, akisisitiza jinsi ushuhuda wa Kikristo katika kukabiliana na mateso daima utafaa kwa mtu wa leo:

“Maudhia ya Wakristo yanayoendelea leo duniani ni jambo linalotuhoji, kwa sababu hata sisi tungeweza kuwa tunahusika, kama vile walivyokuwa Mtakatifu Eulalia, Mtakatifu Pelagius, Mtakatifu Eulogius, na mashahidi wengine wengi ambao masalia yao yamehifadhiwa huku Oviedo. Mashahidi wa mwisho katika jimbo hili walikuwa waseminari wa Oviedo, waliopata ufiadini katika maudhia dhidi ya Kanisa katika miaka ya 30 ya karne iliyopita. Damu ya Wakristo inaendelea kumwagika katika karne ya 21 ili kuweka wazi kwamba, katika Damu ya Kristo, Mungu anatoa msamaha wake bure kwa watu wote.”

Orkestra ya Njia ya Neokatekumenato , iliyotudwa katika hafla hii na wanamuziki 97 na wanakwaya 120, chini ya uongozi ya Tomáš Hanus , mwongoza orkestra maarufu, ilitumbuiza kwa ustadi kazi ya kisimfonia ya Kiko Argüello: Simfonia “Mateso ya Wasio na Hatia” na shairi la kisimfonia “Masiya”.

Tamasha lilizidi matarajio yote; kutokana na shauku ya watazamaji, orkestra ilibidi kucheza vipande kadhaa mara mbili mbili, huku vikisifiwa na wote.

Share: