
Kwa kushirikana na mwaliko wa Baba Mtakatifu Leo XIV katika sala ya Malaika wa Bwana ya Dominika iliyopita:
“Tuinue sala zetu kwa unyenyekevu kwa Bwana ili mlio wa mabomu ukome, silaha zikae kimya, na nafasi kwa ajili ya mazungumzo ifunguliwe”
Kikundi cha Kimataifa cha Wawajibikaji wa Njia, Kiko, Mario na María Ascensión, wanawaalika ndugu wote wa jumuiya za Njia ya Neokatekumenato, kutolea mfungo wao wa Kwaresima na sala zao kwa ajili ya kuiombea amani katika Ijumaa hii tarehe 13 Machi 2026.