
Siku ya Alhamisi, Novemba 13, Padre Mario Pezzi, mpresbiteri wa Kikundi cha Kimataifa cha Njia ya Neokatekumenato, atapokea Shahada ya Udaktari wa Heshima ya Theolojia kutoka Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Mt. Antonio cha Murcia (UCAM).
Heshima hiyo itatotelwa ndani ya hafla ya ufunguzi wa mwaka wa masomo wa 2025-2026, mbele ya Monsinyori José Manuel Lorca Planes, Askofu wa Jimbo la Cartagena-Murcia, María Dolores García Mascarell, Rais wa UCAM, Josefina García Lozano, Mkuu wa Chuo, pamoja na mamlaka mbalimbali za kiraia na kidini na ndugu wengi wa Njia ya Neokatekumenato kutoka Italia na Hispania.
Hafla hiyo, ikitanguliwa na adhimisho la Ekaristi, itajumuisha Laudatio (Wasifu), kuapishwa rasmi na Lectio Magistralis (Fundisho) la Daktari mpya Honoris Causa, Padre Mario Pezzi.

