Onyesho la kimuziki kwa ajili ya Jubilei ya Familia

Kazi ya Kisinfonia ya Kiko Argüello pamoja na Orkestra ya Njia ya Neokatekumenato, ikiwa imeongozwa na Tomáš Hanus Jubilei 2025 Jumapili, Juni 1, 2025, saa moja jioni, katika Ukumbi wa “Parco della Música Ennio Morricone”, kwenye Ukumbi wa Santa Cecilia, Kiko Argüello awasilisha Kazi yake ya Kisinfonia. Onyesho juu kwa ajili ya Jubilei ya Familia, ambapo Orkestra ya Njia ya Neokatekumenato, inayoendeshwa na Tomáš Hanus, mkurugenzi wa Orkestra ya Kisinfonia

Uchaguzi wa Papa Leo XIV

Njia ya Neokatekumenato imepokea habari za kuchaguliwa kwa Kardinali Robert Prevost kuwa Khalifa wa Petro kwa furaha kubwa. Maneno yake ya kwanza yametujaza furaha, akimweka Kristo Mfufuka kama kiini cha yote, ambaye anatupatia amani yake, pamoja na uinjilishaji unaozaliwa kutoka katika moyo wa kimisionari. Kumekuwa na mwangwi wa pekee katika mioyo ya ndugu wote wa Njia—na hasa ule wa kwangu— kutokana na kwamba uchaguzi huu ulifanyika siku ya Bikira Maria

Maaskofu katika Nchi Takatifu wakialikwa na Njia ya Neokatekumenato

Maaskofu na maaskofu wakuu mia mbili na hamsini kutoka mabara matano, wakisindikizwa na wamisionari wasafiri, mapadre na walei, pamoja na kikundi cha wajibikaji wa Njia ya Neokatekumenato katika majimbo yao (jumla ya ndugu zaidi ya 500), walialikwa na kikundi cha kimataifa cha wajibikaji wa Njia -Kiko Argüello, Padre Mario Pezzi na Ascensión Romero- katika mkutano huko Nchi Takatifu. Mwaliko huo kwa Nchi Takatifu ulithibitishwa na barua kutoka kwa Mwadhama Kardinali