Kazi ya Kisinfonia ya Kiko Argüello pamoja na Orkestra ya Njia ya Neokatekumenato, ikiwa imeongozwa na Tomáš Hanus

Jubilei 2025

Jumapili, Juni 1, 2025, saa moja jioni, katika Ukumbi wa “Parco della Música Ennio Morricone”, kwenye Ukumbi wa Santa Cecilia, Kiko Argüello awasilisha Kazi yake ya Kisinfonia. Onyesho juu kwa ajili ya Jubilei ya Familia, ambapo Orkestra ya Njia ya Neokatekumenato, inayoendeshwa na Tomáš Hanus, mkurugenzi wa Orkestra ya Kisinfonia ya Isilandi, itafanya kwa mara ya kwanza, katika jioni hiyo hiyo, kazi mbili za kisinfonia za Kiko: “Mateso ya Wasio na Hatia” na “Masiya“.



Mchoraji mhispania, mwanzilishi wa Njia ya Neokatekumenato pamoja na Carmen Hernández, mtunzi wa kazi muhimu za kiuchoraji, usanifu majengo na wa sanamu mbalimbali ulimwenguni kote, Kiko Argüello anaweka wito wake wa kisanii kwa huduma ya Kanisa na ya Liturujia. Kupitia uchoraji, unaoonyeshwa katika sanaa takatifu na kuakisi nuru ya Mungu, kama vile kupitia muziki, ulio lugha ya kiroho yenye nguvu na ya ajabu, Kiko anapata njia ya kutangaza Injili kwa mtu wa leo. Hivyo, sanaa inachukuliwa kama kielelezo cha uzuri na kama uhusiano wa upendo pmoja na Mungu katika huduma ya Uinjilishaji Mpya.

Katika Mwaka wa Jubilei 2025, tukio hili, chini ulinzi Idara kwa ajili ya Uinjilishaji, litakuwa sherehe kwa manufaa ya familia. Katika bara la Ulaya lililotiwa alama na uduniaisho (upinzani wa dini kwa ujumla), linalishiwa na ukanamungu, linaloathiriwa na hali hafifu ya jamii, utamaduni, kanuni za kimaadili na za kidini, katika enzi yetu ngumu hivi kwa sababu ya ubinadamu uliojeruhiwa kutokana na mateso ya migogoro mingi hivi, “katika kizazi hiki,” alisema Kiko Argüello wakati wa hadhira ya na Papa Fransisko mwaka 2022 kwa ajili ya kutuma familia 430 katika utume. Mungu anaziitia familia, kwa mfano wa Familia ya Nazareti, ili kuleta furaha ya upendo wa Mungu kwa watu ambao bado hawaijui.” Familia, kazi kuu ya sanaa ya Mungu inayouonyesha ulimwengu uzuri wa Kristo na Kanisa lake.

Kazi zake za usanii, maandishi yake, ni wonyesho wa uzuri mpya unaolenga kumsaidia mwanadamu kuinua roho yake kumwelekea Mungu. Muziki wake, pia, kwa namna ya kipekee, hustawisha uvuvio wa kina wa kiroho, hisia ambazo hutuongoza kuelekea ulimwengu wa fumbo la uzuri wa Mungu. Ni sanaa ya kimuziki, iliyovuviwa ili kutia matumaini moyoni mwa mtu anayeteswa, lakini mwenye alama ya hatima ipitayo maumbile ya kawaida.

Mateso ya wasio na hatiani kazi ya kwanza ya Kiko, yenye sehemu tano zilizojikita katika uchungu wa Bikira Maria anayetazama kifo cha Mwanawe. Ni tafakari iliyojaa mvutano mkubwa. Muziki wake wenye ujasiri, pamoja na uimbaji wenye kiasi, vinatusaidia kutafakari fumbo la mateso ambayo inapitia roho ya Mama wa Kristo.

Onyesho hilo lilifanyika kwa mara ya kwanza mnamo 2011 katika Nchi Takatifu, kwenye nyumba ya Domus Galilaeae katika Mlima wa Heri (Korazini, Galilaya), likipitia majukuwa makuu, kumbi za tamasha, maeneo na makanisa makuu ulimwenguni kote: Katedrali ya Madrid, Eneo la Metropolitan huko New York, Chicago Symphony Hall, Berliner Berliner Philharmoniker Hall huko Berlin, jukwaa la Gerard Behar Auditorium huko Yerusalemu, Suntory Hall huko Tokyo, Opera State House ya Jimbo la Hungaria huko Budapest, Memorial Conecert huko Auschwitz (iliyopitishwa kwenye chaneli ya televisheni ya Italia Rai1), Ukumbi wa Paul VI huko Vatikano, Piazza Unità d’Italia huko Trieste…

Baada ya kumaliza sinfonia ya kwanza, Kiko alianza kufanya kazi juu ya nyingine ya pili, ambayo ingetimiza wazo la kimuziki ulio mwendelezo na la kwanza. Safari ya kisanii na ya kiroho ambayo ingempeleka kwenye toleo la mwisho la shairi la kisinfonia linalopigwa na kinanda, kwaya, na okestra, “Masiya,” wimbo wenye sehemu tatu juu ya mateso ya Kristo uliotungwa kwa ajili ya wafiadini.

Vipindi vitatu kutoka katika Historia ya Wokovu vinawekwa katika muziki: Aqedah (“Nifunge”), Binti za Yerusalemu, na Masiya, Simba kwa kushinda. Dhabihu ya Isaka na fumbo la imani ya Abrahamu, maneno ya Kristo kwa wanawake wanaomfuata katika Via Dolorosa (Njia ya Mateso), maneno ya kishairi ya Mt. Victorinus wa Pettau, mkristo mfiadini wa karne ya 4, anayetangaza Fumbo la Kristo, aliye “simba” wa kushinda, lakini ambaye anajifanya mwana-kondoo ili ateseke. Vilionyeshwa kwa mara ya kwanza mnamo Novemba 19, 2023, katika Jumba la Teatro Verdi huko Trieste na ilionyeshwa kwenye Rai5, chaneli ya muziki na sanaa ya Rai Cultura.

Onyesho hilo litaonekana kwa njia mubashara katika nchi 137 na litapatikana kwenye tovuti hii rasmi ya Njia ya Neokatekumenato.

Njia ya Neokatekumenato Orkestra ya Kisinfonia
Orkestra ya Kisinfonia ya Njia ya Neokatekumenato
Share: