Picha na madirisha

Michoro katika Njia ya Neokatekumenato
Kiko Argüello alisomea Sanaa katika Chuo cha Mt. Fernando cha Madrid na mwaka 1959 alipokea Tuzo ya Kitaifa ya Pekee ya Uchoraji. Mnamo 1960, pamoja na mchongaji sanaa Coomontes na mchoraji wa vioo Muñoz de Pablos, alianzisha kikundi cha utafiti na maendeleo ya Sanaa Wakfu “Gremio 62”. Alifanya maonyesho huko Madrid (Maktaba ya Taifa), na kuiwakilisha Hispania, akiteuliwa na Wizara ya Utamaduni, katika Maonyesho ya Sanaa Takatifu Ulimwenguni huko Royan (Ufaransa) mwaka wa 1960. Huko Uholanzi, alionyesha baadhi ya kazi zake (Nyumba ya sanaa “Sura mpya”).
Taji la Kifumbo

“Uzuri mpya peke yake utaokoa Kanisa». Picha za “taji la kifumbo” hili zinataka kupenya mpaka ndani kabisa ya roho ya mwumini azitazamazo. Zimekusudiwa kumsaidia mwanadamu kumuinukia Mungu. Picha hizi zinatenda juu rohoni mwa Mkristo kama kwenye Kugeuka Sura, ambapo mitume waliona mng’ao wa mwanga wa kimungu juu ya Mlima Tabori. Kama yeye, wanasikiliza Neno la Mungu, na zaidi ya yote katika liturjia, picha hizi, kwa njia ya moja kwa moja, hapo hapo na kwa hisia zaidi, zinataka kuwasaidia waumini kugeuka sura kiroho. Mtakatifu Yohane wa Dameski, ambaye alitetea michoro hii dhidi ya nguvu ya “iconoclasm” (mkondo uliokataza na kuharibu picha za kidini) na ambaye Papa Leo XIII alimtangaza kuwa Mwalimu wa Kanisa Zima, alisema: “Nimeona sura ya kibinadamu ya Mungu na nafsi yangu imeokolewa”
Sura Takatifu ya Kristo iwasaidie ninyi kuwa mashahidi wa upendo wake.
Kiko Argüello.
Usanifu Majengo
Usanifu Majengo katika Njia ya Neokatekumenato

Katika historia, Kanisa daima limekuwa na kifungo hiki kati ya uzuri na uinjilishaji, nalo Kanisa limekuwa mjumbe mkubwa zaidi wa uzuri. Kila kitu kinaakisi uzuri wa Kristo na uzuri wa jumuiya na wa ushirika wa kindugu. Uinjilishaji wa mataifa ya Waslavi (“Slavonic peoples”) ulifanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa njia ya uzuri wa liturjia, wa picha na nyimbo. Ni katika miaka hii ya mwisho tu ambapo hata ndani ya Kanisa maono ya kitendaji yanaonekana kutawala ambayo yanapunguza mahali ambapo jumuiya inaishi na kukutana kuwa tu vyumba vya mikutano mkutano.
Walakini, hasa leo, zaidi kuliko hapo awali ni lazima na ya dharura kwamba miundo ya Kanisa ifanywe upya. Jibu kwa utandawazi (kijiji cha ulimwengu), kwa jiji kubwa, kwa “utamaduni mmoja”, ni parokia ambayo inakuwa “kijiji cha mbinguni”: mfano wa kijamii wa kibinadamu zaidi wenye uwezo wa kufungua nafasi kwa ajili ya jamii mpya ya upendo Kusanyiko la Ekaristi linalowawezesha waumini kushiriki kwa namna hai, uhalisia wa jumuiya ya jumuiya zenye “catecumenium” inayoundwa na kumbi za kupendeza za kiliturjia kwa maadhimisho katika jumuiya ndogo.
Katika mabara yote matano inawezekana kukutana na kazi zilizofanywa na Kiko ndani ya uzuri mpya: Seminari za Redemptoris Mater, parokia mpya, “catecumenium” (yaani, kumbi kwa maadhimisho ya jumuiya), nk.
Uchongaji sanaa
Uchongaji sanaa katika Njia ya Neokatekumenato

Dostoevsky, “Uzuri utaokoa ulimwengu.” Uzuri, kama mnavyojua, ni silka ya utu, pamoja na wema na ukweli. Kwa sababu, kama anavyosema Mtakatifu Thomaso, uhalisia wote ni mmoja, ni wa kweli, ni halisi. Lakini mimi ninapenda kuhusisha uzuri na raha. Hisia ya uzuri, urembo, hutupatia raha, hutufanya tusikie hisia. Kwa hiyo Mungu, kwa namna fulani, ameumba maumbile. Aliyeumba maumbile, ameyafanya kuwa mazuri ili kutupatia raha.
Raha inahusiana na upendo. na inavutia, kwangu mimi kama mchoraji, niliyesomea sheria za uwiano, kwamba kila kitu katika maumbile kinahusiana na uzuri, na kipo kwa ajili ya uzuri. Si kila kitu ni uzuri, kwa maana fulani, lakini sheria za uwiano zinahusiana katika maada, katika umbo… Inaamsha shauku, sayansi inayosoma mahusiano ni hisabati, ndiyo maana katika uwiano kuna mfuatano mzima wa milinganyo ambayo ni ya kihisabati. Tayari katika sanaa ya Plato alizungumza juu ya jiometria ya uumbaji na ya hisabati. Katika sanaa, iwe katika uchoraji, iwe katika uchongaji, iwe katika muziki, iwe katika ushairi, kila kitu kiko kwenye uhusiano, mahusiano ambayo yanapatana.

Uhusiano huu wa kihisabati uliopo katika uwiano, upo vilevile katika wakati, upo katika muziki. Muziki ni muhimu sana kwa sababu unatufundisha uzuri katika mgawanyiko wa muda. Kila nota inatoa thamani ya nota inayofuata katika wakati, katika uchoraji kila kitu, kila mumbile , kila nyenzo, kila mchoro unathamini mwingine. Kwa mfano, simfonia ya nne ya Beethoven, inaanza na “dissonance” (nota zisizoendana). Ni ajabu. Kuthamini muda ndani ya wakati, tuseme kwamba kuna … Tusiseme juu ya ushairi, neno, uchongaji. Kwa mfano, Henry Moore, mchongaji sanaa mwingereza, amesomea mifupa ya mwanadamu, na ameona kwamba mifupa ya mtu … Pengo ndani ya mfupa wa paja ni kamilifu. Pengo hilo ni kamilifu kwa ajili ya kazi ya uungaji wa mifupa na wakati huo huo unapendeza, hadi kiwango cha juu. Kutengeneza tao lenye uzuri, linalopendeza, ni vigumu sana. Tao la shingo ya sili ni ya ajabu. Jinsi wanyama wanavyohusiana, sio kila tao lina uzuri. Moore anachukua mapengo haya, anayasoma na kutengeneza sanamu yenye matao, kwa sababu tao la aina fulani linaendana na uvimbe mwingine wa aina nyingine ili kuleta uzuri, kwa sababu kila kitu kinahusiana.
Tuseme hivi kwamba katika uzuri kuna siri ya kina, ambayo ni upendo.
Kiko ametengeneza vifaa vingi kwa ajili ya liturjia: vikombe, sahani, vyetezo, vifuniko vya Biblia, mapambo…, na pia sanamu nyingi: Hotuba ya Mlimani, Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili, Yesu Kristo msulubiwa, paa nk.
Vitabu
Wasifu wa Maisha – Carmen Hernández
Kununua
Katika maelezo haya ya wasifu mtamwona mwanamke wa kipekee, muhimu sana kwa Kanisa, aliyeshikwa upendo na Kristo, na Maandiko na pia na Ekaristi. Alijua wazi kwamba utume ambao Mungu alikuwa amempa ulikuwa kuniunga mkono, kunitetea na kunisahihisha, kwa manufaa ya Njia ya Neokatekumenato. Ninamshukuru Mungu kwa ajili ya Carmen ambaye daima ameniambia ukweli. Alikuwa mwanamke wa kina, halisi na huru katika uhusiano wake na kila mtu. Alikuwa na akili sana. Alimpenda Kristo na Kanisa na Papa, zaidi ya yote. Tunaamini kwamba Carmen yuko pamoja na Bwana, tayari yuko kwenye sherehe. Maelezo haya ya wasifu si tu kwa ajili ya ndugu wa Njia, bali ni kwa ajili ya Kanisa zima, kumtambulisha mwanamke wa ajabu, ambaye ameishi imani kwa kiwango cha kishujaa. Carmen Hernandez! (Kiko Arguello).
Wasifu rasmi wa kwanza wa Carmen Hernández umechapishwa. Kumbukumbu ya miaka mitano ya kufariki kwake Carmen Hernández, Julai 19, 2021, inalingana na kuchapishwa kwa wasifu wake rasmi wa kwanza, ambaye mwandishi wake ni profesa na daktari wa Falsafa Aquilino Cayuela na umehaririwa na Maktaba ya Waandishi wa Kikristo (BAC).
Kerigma. Katika vibanda pamoja na maskini.
Kununua
“Nimetaka kuandika kitabu hiki kidogo kilichopendekezwa na Kardinali Cañizares, ambaye aliona ni muhimu niseme kitu kuhusu yale ambayo Bwana amefanya nasi katika vibanda, pamoja na maskini, na pia kwamba ningechapisha kerigma ambayo itaweza kusaidia, hasa kwa upande wa maudhui na wa anthropolojia, kwa ajili ya Sinodi juu ya Uinjilishaji Mpya». Kiko Arguello.
Kardinali Cañizares: «Kitabu hiki ni zawadi kweli ya Mungu, kinachotuhuisha na kututia moyo katika imani, kinachoondoa hofu na kutujaza ujasiri.
Kardinali Schönborn: “Katika katekesi hii, kwa namna ya ajabu, tangazo zima la Injili limefupishwa”.
Noti 1988-2014
Kununua
“Tangu karibu miaka thelathini iliyopita, nimekuwa nikiandika kwenye daftari, mara kwa mara na bila utaratibu, na bila nia iliyodhamiriwa, baadhi ya mawazo, tafakari, kweli, kumbukumbu, fikira, maelezo, mazungumuzo ya nafsi, maombi, n.k., yaliyoamshwa ndani yangu wakati wa utume wa uinjilishaji na wa katekesi ambayo kwayo Bwana ameniita katika Kanisa, pamoja na Carmen Hernández na Pd. Mario Pezzi. Ikiwa noti hizi zinamsaidia mtu, Mungu na ahimidiwe”.
“Kitabu hiki kimeundwa na vipande vidogo vya fasihi ambavyo vinaweza kusomwa bila kuunganishwa na kile kilichotangulia au kinachofuata. Ni tafakari zilizotokana na tukio, kuishi pamoja au mkutano; kubisha mlango wa roho kwa kutangaza au kujishtaki; kujiuliza au kujiita kwa matumaini ambako msomaji anajisikia kuhusishwa: mara nyingi ni siri za kuthubutu zinazotoka katika nafsi ya mwandishi; wakati mwingine ni aina ya tenzi au zaburi, dua zenye moto na shukrani za kusisimua kwa Mungu. Kwa maelezo yaliyomo kwenye maandishi mafupi haya inawezekana kwa namna fulani kufuata mkondo wa kihistoria kutoka 1988 hadi 2014. Yanaunganishwa na historia ya imani ya mwandishi na ya Njia ya Neokatekumenato, zaidi kuliko uendelezaji wa mada, ingawa maudhui mengi ya karama husika yanaonekana hapa na pale. Ni historia iliyojaa furaha na mateso; inaruhusu kuona pambano la mwandishi kwa kutekeleza kwa uaminifu agizo lililopokelewa kutoka kwa Mungu» († Mons. Ricardo Blázquez Pérez, Kardinali Askofu Mkuu wa Valladolid).
Shajara za 1979-1981
Kununua
“Kunanyesha, lakini siku inapambazuka tulivu. Yesu, nashangaa. Asante. Mateso yameweka huruma moyoni mwangu. Asante Yesu. Amani, furaha…”. Carmen Hernández, Bonde la Walioanguka – Madrid, Januari 27 kutoka 1979.
“Miaka hamsini bila kusimama hata mara moja, safari, uchunguzi, kutembelea jumuiya nyingi huko Madrid, Zamora, Barcelona, Paris, Roma, Florence, Ivrea… Kusikiliza na kusikiliza kila ndugu kuhusu maisha yake, mateso yake na historia yake, ikiangazwa kwa nuru ya imani, ya msalaba mtukufu wa Bwana Wetu Yesu. Nafikiri kwamba mna haki ya kuufahamu moyo wake Carmen, upendo wake mkuu kwa Yesu Kristo. Alisema mara daima: “Yesu wangu, nakupenda, nakupenda. Njoo, njoo, nisaidie»» (Kiko Argüello).
Njia ya Neokatekumenato

Maneno ya Mapapa: Paulo VI, S. Yohane Paulo II, Benedikto XVI na Fransisko.
Mitume wa kwanza, katika vikundi vidogo vya uinjilishaji, walizunguka katika masinagogi wakitangaza Habari Njema: Mungu amemfufua mtumishi wake Yesu, ambaye sisi tumemkana, tukiomba neema kwa mwuaji; yule aliyekufa bila kuweka pingamizi, bila kushindana na uovu, akiwapenda adui zake, asiwahesabie makosa (“Wasamehe kwa sababu hawajui watendalo”); yule aliyetoa sadaka mabaya waliyomfanyia -mateso na msalaba – kama uthibitisho wa kwamba upendo wake ulikuwa mkubwa kuliko mauti na kwamba hakuacha kuwapenda, hata kama wangechukua uhai wake: Mungu alimfufua kutoka mauti na leo Yeye yu hai, ili kusamehe kosa hili na lingine lolote.
“Muda wetu unahitaji kuanza upya ujenzi wa Kanisa, karibu kisaikolojia na kichungaji, kana kwamba lingeanza tena, kutoka mwanzo, kwa kusema hivi, kuzaliwa upya» Paul VI, Hotuba ya Jumatano, Agosti 4, 1976.
Nyimbo za Njia ya Neokatekumenato

Imepitiwa na Senta ya Neokatekumenato ya Jimbo la Madrid. Kitabu cha nyimbo kimehaririwa kwa rangi mbalimbali ili kutofautisha hatua za mihula ya Njia. Waimbaji wanapswa kuchagua nyimbo kulingana na hatua ya Njia ambamo Jumuiya yao imo na kusubiri makatekista wawapitishie nyimbo katika Kuishi Pamoja mbalimbali na Hatua za Njia, kwa njia hii ndugu wanaweza kuelewa maana ya kila wimbo.
Orkestra
Orkestra ya Kisimfonia ya Njia ya Neokatekumenato imeanzishwa kama huduma ya Njia ya Neokatekumenato kwa uinjilishaji kupitia muziki.
