Kutumwa kwa Missio ad gentes tarehe 1 Februari 2014

21 Aprili 2025

Kiko, Padre Mario na Ascensión, wajibikaji duniani wa Njia ya Neokatekumenato, pamoja na Ndugu wote wa Njia wamepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Baba Mtakatifu, Papa wetu Fransisko.

Jana, katika ujumbe wake wa Pasaka Urbi et Orbi (maana yake “kwa mji (Roma) na kwa dunia nzima”), ametupatia ushuhuda wake wa mwisho wa imani: Ndugu wapendwa: Katika Pasaka ya Bwana, kifo na uzima zimekabiliana katika pambano la ajabu, lakini Bwana yu hai milele na anatupatia uhakika wa kwamba sisi pia tumeitwa kushiriki katika uzima usio na mwisho, ambapo hazitasikika tena kelele za silaha, wala miangwi ya kifo. Tujikabidhi kwake Yeye, kwa sababu Yeye peke yake anaweza kuvifanya vitu vyote kuwa vipya”.

Tunamshukuru Bwana kwa kutupatia aliyejaa mwenye ari, aliyeifikisha Injili katika nyanja za mbali zaidi za Kanisa, akijitoa ili kudhihirisha ukaribu na upendo wa Mungu kwa wote, hasa kwa walio maskini na kutelekezwa zaidi mwilini na rohoni. Tunahifadhi moyoni mwetu, kwa shukrani, ushuhuda wake wa kujitoa kikamilifu kushuhudiaupendo wa Mungu kwa kila kiumbe.

Tangu mwanzoni mwa Upapa wake mwaka 2013, Njia imejisikia kuungwa mkono na kutegemezwa na Papa Fransisko. Katika mikutano mbalimbali ambayo tumekuwa nayo kwa miaka hii, ametuonyesha daima ukaribu wake kama Baba, nasi tumempenda. Hasa, tunafurahi kukumbuka kutumwa kwa familia nyingi za Njia katika utume kwa mabara tofauti tofauti, pamoja na maneno yake katika tukio la kuadhimisha miaka 50 ya Njia ya Neokatekumenato, Mei 5 2018: Ndugu na dada wapendwa, karama yenu ni zawadi kubwa ya Mungu kwa Kanisa la wakati wetu. Tumshukuru Bwana kwa miaka hii hamsini… Ninawasindiza na kuwahimiza: Songeni mbele!

Tunawaomba ndugu wote wa Njia ya Neokatekumenato kumwombea Baba Mtakatifu. Tumwombe Bwana amkaribishe katika amani ya Ufalme wake.

Kristo amefufuka! Kwelikweli amefufuka!


Hadhira binafsi ya Kikundi cha Kimataifa na Papa Fransisko tarehe 19 Aprili 2018
Share: