Papa Fransisko alimpigia simu mwanzilishi wa Njia ya Neokatekumenato, Kiko Argüello, alasiri ya tarehe 9 mwezi Januari ili kumpongeza kwa kutimiza miaka 81 ya uhai.
Fransisko alitumia fursa hiyo kwa ajili ya kumsalimia na kumwahidia kwa mara nyingine tena kwamba atamtegemeza yeye pamoja na Njia nzima ya Neokatekumenato, akimhimiza kuendelea kusonga mbele. Kiko, akishangazwa na zawadi hiyo kutoka kwa Baba Mtakatifu, alimshukuru sana kwa tendo hilo na alifanya upya utii wake na heshima yake kwake.
Isitoshe, mwanzilishia wa Njia alimhakikishia kwamba atamwombea katika huduma yake.
