Njia ya Neokatekumenato na Jubilei

Ushuhuda wa Kiko Argüello. Pentekoste 2025 Naitwa Kiko Argüello na, pamoja na Mtumishi wa Mungu, Carmen Hernández, sisi ni waanzilishi wa Njia ya Neokatekumenato, utaratibu wa kijimbo wa uingizwaji wa kikristo ambao – kupitia katekesi, Neno la Mungu na sakramenti zinazoshirikiwa katika jumuiya – huwaongoza watu kuishi imani kipevu na ushirika wa kindugu. Mimi ni mchoraji mhispania. Wakati wa miaka yangu ya chuo kikuu, baada ya dhahama kubwa ya kiutu,

Papa Fransisko ampongeza Kiko Argüello kwa kutimiza miaka 81 ya uhai

Papa Fransisko alimpigia simu mwanzilishi wa Njia ya Neokatekumenato, Kiko Argüello, alasiri ya tarehe 9 mwezi Januari ili kumpongeza kwa kutimiza miaka 81 ya uhai. Fransisko alitumia fursa hiyo kwa ajili ya kumsalimia na kumwahidia kwa mara nyingine tena kwamba atamtegemeza yeye pamoja na Njia nzima ya Neokatekumenato, akimhimiza kuendelea kusonga mbele. Kiko, akishangazwa na zawadi hiyo kutoka kwa Baba Mtakatifu, alimshukuru sana kwa tendo hilo na alifanya upya utii