Kimechapishwa kitabu kipya kuhusu Carmen, mwanzilishi mwenza pamoja na Kiko  Argüello wa Njia ya Neokatekumenato, na kinastahili kuzingatiwa nasi. Tunsaema kuhusu kitabu kinachoitwa Corazón Indiviso, misión y virginidad en Carmen Hernández, (“Moyo Usiogawanyika, utume na ubikira katika Carmen Hernández”) iliyoandikwa na Josefina Ramón, mshiriki katika Njia wa Neokatekumenato, na ambaye, kwa kufuata nyayo za Carmen, ni pia mseja na mmisionari msafiri, na kwa kuwa alilishwa na maisha na utajiri wa mawazo ya Carmen Hernández, sasa anatupakulia mawazo yayo hayo, kupitia kitabu kiki, kama chakula chenye lishe bora.



Share: