Sala kwa ajili ya Papa Benedict XVI

Madrid, 29 Desemba 2022 Ndugu wapendwa: Papa Fransisko, kwenye hadhira yake kuu Jumatano iliyopita, ameliomba Kanisa zima la Ulimwengu kuinua maombi kwa ajili ya Papa Mstaafu Benedict XVI, ambaye afya yake imedhoofika sana katika siku za hivi karibuni. Sisi ndugu wa Njia ya Neokatekumenato tunajiunga na ombi hili. Ni kiasi gani tunachopaswa kumshukuru Papa Benedict kwa upendo wake kwa ajili ya Njia, uliodhihirishwa katika matukio mengi mbali mbali! Tusali pamoja