Benedict XVI, Kiko Argüello, Carmen Hernández  na Pd. Mario Pezzi hadhira

Madrid, 29 Desemba 2022

Ndugu wapendwa:

Papa Fransisko, kwenye hadhira yake kuu Jumatano iliyopita, ameliomba Kanisa zima la Ulimwengu kuinua maombi kwa ajili ya Papa Mstaafu Benedict XVI, ambaye afya yake imedhoofika sana katika siku za hivi karibuni.

Sisi ndugu wa Njia ya Neokatekumenato tunajiunga na ombi hili. Ni kiasi gani tunachopaswa kumshukuru Papa Benedict kwa upendo wake kwa ajili ya Njia, uliodhihirishwa katika matukio mengi mbali mbali! Tusali pamoja na Baba Mtakatifu Fransisko na Kanisa zima katika nyakati hizi ili Bwana amtegemeze mtumishi wake mwaminifu katika hali hii ya mpito.

Tunawaomba, ndugu wapendwa, tuinue sala kwa ajili ya Papa wetu mpendwa Benedict katika ibada za siku hizi zijazo.

Mtuombee na sisi pia.

Kiko, Pd. Mario na Ascensión

Share: