Kanisa la Fuentes de Carbonero

Mahali pa kuhiji na kuadhimisha, ushuhuda wa historia ambayo Mungu hufanya pamoja nasi.

Njia ya Neokatekumenato Kanisa la Kupalizwa Bikira Maria huko Fuentes de Carbonero - Segovia - Hispania wakati wa ukarabati, mwaka 2021

«Nilishangaa sana kwamba wakati nyumba zote katika kijiji hicho ziliharibika, kitu pekee kilichobaki kikisimama katika kijiji hicho kilichotelekezwa kilikuwa kanisa, na kanisa ambalo limejaa maskini.Hapa tulisherehekea Mkesha wa Pasaka na ndugu wa vibandani na wale wa jumuiya ya kwanza ya Madrid. Hatukuwa na umeme; Tulijiangazia na nuru ya mshumaa mkubwa wa zamani tulioukuta. Kulipopambazuka tulikula mwana-kondoo tuliyekuwa tumeagiza huko Carbonero»

Kiko Argüello.
Ukarabati wa Kanisa la Fuentes
Njia ya Neokatekumenato Kiko Argüello katika Kanisa la Kupalizwa Bikira Maria huko Fuentes de Carbonero - Segovia - Hispania

Oktoba 12 iliyopita (2022), sikukuu ya Bikira wa Pilar (Bikira wa Nguzo) huko Fuentes de Carbonero el Mayor, kijiji kidogo karibu na Segovia kilichotelekezwa na watu tangu 1960, ilitukia sherehe yenye kwa kweli maana ya pekee mno.

Ekaristi iliongozwa na Askofu wa Segovia, Mhashamu Mons. Askofu César Franco, akisindikizwa na mapadre zaidi ya thelathini na wakiwepo kama watu 500 waliojaza kanisa hilo na eneo linalolizunguka.

Licha ya kanisa dogo ambalo sasa limekarabatiwa kikamilifu kutokana na juhudi na kazi zilizotekelezwa na Njia, eneo hilo limezungukwa na mashamba.

Ni nini cha upekee kuhusu mahali hapa? Kwa nini kanisa limejengwa upya mahali palipoachwa na watu na ambalo lingefikiriwa pia kutelekezwa na mkono wa Mungu?

Mahali pa kuhiji

Ili kutembelea Fuentes, ombi kupitia barua pepe kwa:

Ukionyesha siku na saa unayotamani na idadi ya wahiji. Barabara ya kufikia na maegesho ni madogo sana, kwa hivyo ni lazima kufanya ‘booking’ ya siku na saa ya ziara.

Njia ya Neokatekumenato Kanisa la Kupalizwa Bikira Maria huko Fuentes de Carbonero - Segovia - Hispania, mwaka 1965
Kiko Argüello na Fuentes

Kilomita mbili kutoka mji wa Carbonero el Mayor (Segovia) ni Fuentes de Carbonero. Tangu 1960, kijiji hicho hakina wakazi na hekalu pekee ndilo lililobaki.

Njia ya Neokatekumenato Kiko Argüello kwenye kisima katika Kanisa la Kupalizwa Bikira Maria huko Fuentes de Carbonero - Segovia - Hispania
Kisima cha Fuentes

«Mungu ametaka kwamba, katika mwaka wa 1965, nikitamani kupata mahali pa mafungo na sala, nilikuta kanisa la Fuentes de Carbonero likiwa limetelekezwa. Nilipokuwa nikitembea nyanda tambarare za Kastiya siku yenye mawingu, mwali wa jua uliangazia madini ya ulanga ambayo yalienea katika eneo hilo na ghafla kila kitu kiliangazwa na nilivutiwa kabisa: kanisa kwenye uwanda ule wazi lilikuwa ni tokeo halisi la kimungu. Lilikuwa wazi na tupu; bado lilikuwa na baadhi ya picha na sanamu nyuma ya altare; sakristia ilikuwa na jukwaa la mbao iliyonisaidia mimi kulala. Nilibaki nikiishi huko siku kumi na tano, nikisali peke yangu na kwa matunda makubwa. Kwa kuona kwamba palikuwa mahali pazuri ajabu, nilirudi hapo mara kadhaa, nikiishi peke yangu, katika kufunga na kusali, na nikilala na mfuko wangu wa kulalia katika sakristia»

Kiko Argüello.
Kesha la Pasaka
Njia ya Neokatekumenato Carmen Hernández huko Fuentes de Carbonero - Segovia - Hispania
Carmen Hernández huko Fuentes kipindi cha joto mwaka huo

«Kwa kuwa mto fulani ulipita karibu na hapo, niliamua kuwachukua akina ndugu kutoka vibandani kwa siku chache wakati wa kiangazi ili na wao pia wapate likizo. Tuliishi wiki ya mapumziko, ushirika na upendo. Mwaka 1967 tuliadhimisha Mkesha wa Pasaka katika kanisa la Fuentes pamoja na ndugu kutoka Palomeras na wale wa parokia ya kwanza ya Madrid. Mnamo 1969 nilimwambia Pd. Fransisko Cuppini – padri wa kwanza ambaye alitusindikiza Carmen na mimi- aje nami kuishi Juma Takatifu. Tulikwenda huko, wala hatukuwa na umeme, lakini kulikuwa na mshumaa mkubwa wa zamani na tuliuwasha. Tuliagiza mwana-kondoo kutoka kijiji jirani kwa ajili ya karamu ya Pasaka, alfajiri yake. Tulisherehekea Mkesha wa Pasaka bila umeme; Pd. Fransisko Cuppini aliuongoza»

Kiko Argüello.
Uinjilishaji

«Pia ilikuwa huko Fuentes ambapo Mkutano wa kwanza wa makatekista wasafiri ulifanyika na kutoka hapo vikundi vya kwanza kwa ajili ya Amerika waliondokea kwenda kuinjilisha»

Kiko Argüello.
Njia ya Neokatekumenato Kiko Argüello na Carmen Hernández katika Kanisa la Kupalizwa Bikira Maria huko Fuentes de Carbonero - Segovia - Hispania
Kiko Argüello na Carmen Hernández en Fuentes en 1969

Kuishi pamoja hiyo ya kwanza, iliyoitishwa na Kiko na Carmen, ilifanyika kuanzia Agosti 1 hadi 20, 1969, mwaka mmoja baada ya Njia ya Neokatekumenato kuanzishwa huko Italia.

Tangu hapo, njia hii mpya ya uingizwaji wa kikristo, muundo wa kikatekesi unaojikita katika Neno la Mungu, Liturjia na Jumuiya, umeenea kwa kasi katika Hispania na Italia, na sasa ipo duniani kote.

Kiti Kitakatifu kiliziidhinisha kanuni (‘Statuta’) za Njia ya Neokatekumenato mnamo 2008.


Pakua kipeperushi
Share: