Njia ya Neokatekumenato na Jubilei

Ushuhuda wa Kiko Argüello. Pentekoste 2025 Naitwa Kiko Argüello na, pamoja na Mtumishi wa Mungu, Carmen Hernández, sisi ni waanzilishi wa Njia ya Neokatekumenato, utaratibu wa kijimbo wa uingizwaji wa kikristo ambao – kupitia katekesi, Neno la Mungu na sakramenti zinazoshirikiwa katika jumuiya – huwaongoza watu kuishi imani kipevu na ushirika wa kindugu. Mimi ni mchoraji mhispania. Wakati wa miaka yangu ya chuo kikuu, baada ya dhahama kubwa ya kiutu,

Papa Leo XIV ampokea Kiko Argüello, mwanzilishi wa Njia ya Neokatekumenato

Leo asubuhi, tarehe 5 Juni 2025, saa tano asubuhi, katika Maktaba ya Ikulu ya Kitume, Baba Mtakatifu Leo XIV amepokea kwa mara ya kwanza kwa faragha Kikundi cha Kimataifa ya Njia ya Njia ya Neokatekumenato, Kiko Argüello, Padre Mario Pezzi, na María Ascensión Romero. Kiko alimsalimia Papa, akimwambia kwamba alikuwa na furaha sana kwamba Mungu ametupa Papa mmisionari, kwa sababu hii pia ndio utume wa Njia ya Neokatekumenato, katika nchi