Maadhimisho ya Miaka 60 ya Njia ya Neokatekumenato na Tukio la Kufungwa kwa Awamu ya Kijimbo ya Mchakato wa Kumtangaza Carmen Hernández kuwa Mtakatifu

Madrid. Kardinali Cobo Cano ataongoza Misa Takatifu katika maadhimisho ya miaka 60 ya Njia ya Neokatekumenato na Tukio la kufunga awamu ya kijimbo ya mchakato wa kumtangaza Mtumishi wa Mungu Carmen Hernández kuwa mwenye heri. Siku ya Jumamosi, Mei 30, saa 2:00 usiku, Kardinali José Cobo Cano, Askofu Mkuu wa Madrid, ataongoza adhimisho la Ekaristi katika Kathedrali ya Bikira Maria Mama Yetu wa Almudena, ili kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 60

Sala kwa ajili ya Amani

Kwa kushirikana na mwaliko wa Baba Mtakatifu Leo XIV katika sala ya Malaika wa Bwana ya Dominika iliyopita: Kikundi cha Kimataifa cha Wawajibikaji wa Njia, Kiko, Mario na María Ascensión, wanawaalika ndugu wote wa jumuiya za Njia ya Neokatekumenato, kutolea mfungo wao wa Kwaresima na sala zao kwa ajili ya kuiombea amani katika Ijumaa hii tarehe 13 Machi 2026.

Njia ya Neokatekumenato: “Mchango wenye thamani kwa maisha ya Kanisa”

Mmewasha moto wa Injili pale ambapo ulionekana kuzimika.  Papa Leo XIV Papa Leo XIV akutana na Makatekista 1.000 kutoka Njia ya Neokatekumenato Asubuhi ya leo, 19 Januari 2026, Baba Mtakatifu Leo XIV, katika “Ukumbi wa Baraka” aliwapokea makatekista wasafiri zaidi ya 1,000, wawajibikaji wa Njia ya Neokatekumenato katika mataifa 138 katika mabara yote matano. Mwishoni mwa kuishi pamoja, iliyofanyika katika Kituo cha “Mtumishi wa Yahweh” huko Porto San Giorgio (Italia),