Sala kwa ajili ya Amani

Kwa kushirikana na mwaliko wa Baba Mtakatifu Leo XIV katika sala ya Malaika wa Bwana ya Dominika iliyopita: Kikundi cha Kimataifa cha Wawajibikaji wa Njia, Kiko, Mario na María Ascensión, wanawaalika ndugu wote wa jumuiya za Njia ya Neokatekumenato, kutolea mfungo wao wa Kwaresima na sala zao kwa ajili ya kuiombea amani katika Ijumaa hii tarehe 13 Machi 2026.

Njia ya Neokatekumenato: “Mchango wenye thamani kwa maisha ya Kanisa”

Mmewasha moto wa Injili pale ambapo ulionekana kuzimika.  Papa Leo XIV Papa Leo XIV akutana na Makatekista 1.000 kutoka Njia ya Neokatekumenato Asubuhi ya leo, 19 Januari 2026, Baba Mtakatifu Leo XIV, katika “Ukumbi wa Baraka” aliwapokea makatekista wasafiri zaidi ya 1,000, wawajibikaji wa Njia ya Neokatekumenato katika mataifa 138 katika mabara yote matano. Mwishoni mwa kuishi pamoja, iliyofanyika katika Kituo cha “Mtumishi wa Yahweh” huko Porto San Giorgio (Italia),

Nuru ya Bikira Maria Mkingiwa yang’aa huko Oviedo

Njia ya Neokatekumenato inaadhimisha kumbukumbu ya miaka 50 huko Oviedo (Hispania) kwa uwepo wa Kiko Argüello na Askofu Mkuu Mha. Jesús Sanz Montes. Tamasha huko Oviedo Ili kuadhimisha miaka 50 ya Njia ya Neokatekumenato huko mkoani Asturias, katika mji wa Oviedo, Askofu Mkuu Mons. Jesús Sanz Montes aliongoza Mkesha wa Sherehe ya Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili pamoja na jumuiya za Neokatekumenato za mji huo mkuu Mkoa wa Asturias.

Shahada ya Udaktari wa Hesima (“Honoris causa”) yatolewa kwa Pd. Mario Pezzi

Siku ya Alhamisi, Novemba 13, Padre Mario Pezzi, mpresbiteri wa Kikundi cha Kimataifa cha Njia ya Neokatekumenato, atapokea Shahada ya Udaktari wa Heshima ya Theolojia kutoka Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Mt. Antonio cha Murcia (UCAM). Heshima hiyo itatotelwa ndani ya hafla ya ufunguzi wa mwaka wa masomo wa 2025-2026, mbele ya Monsinyori José Manuel Lorca Planes, Askofu wa Jimbo la Cartagena-Murcia, María Dolores García Mascarell, Rais wa UCAM, Josefina

“Tuzo Maalum ya Mwaka” katika gazeti la kidijitali “Religión en Libertad” yatolewa kwa Kiko Argüello

Jumatano tarege 29 Oktoba 2025 (Madrid, Hispania) RATIBA 19:30: Mwanzo wa hafla. Utambulisho kutoka kwa Álex Navajas na Sandra Segimon. Kukabidhi tuzo: 20:45: Mwisho wa hafla na wageni waalikwa kuagwa.

Ufafanuzi wa Njia ya Neokatekumenato + Nyongeza

Njia ya Neokatekumenato ni safari ya malezi ya kikatoliki inayotekelezwa katika majimbo kupitia huduma za bure (taz. Kifungu cha 4 cha Statuta za Njia ya Neokatekumenato), iliyoidhinishwa na Kiti Kitakatifu. Mikusanyiko ya maadhimisho ya jumuiya hutumia nyenzo mbalimbali (nyimbo, ishara za kiliturujia na michoro), ambazo ni matunda ya ubunifu wa Kiko Argüello na Carmen Hernández, ambao, bila kutafuta faida, wamezifanya zipatikane bila gharama yoyote kwa ndugu wa jumuiya na parokia