
Alasiri ya Mei 26, Jumapili ya Utatu Mtakatifu, mkutano ulifanyika katika Senta ya Neokatekumenato huko “La Pizarra” (El Escorial, Hispania) na Kadinali José Cobo, Askofu Mkuu wa Madrid, na Kikundi cha Wawajibikaji Kimataifa wa Njia ya Neokatekumenato, ambacho kwa sasa kimeundwa na Kiko Argüello – mwanzilishi mwenza wa mkondo huu wa kanisa. pamoja na Mtumishi wa Mungu Carmen Hernández – Padre Mario Pezzi na Ascensión Romero, huku wakisindikizwa na ndugu wapatao 700 kutoka jumuiya za Jimbo la Madrid -waliowakilisha jumuiya 222 zilizopo katika parokia 44 katika Jimbo hilo- wakiwemo watoto wapatao 100 – watoto wao – na mapadre wapatao 70, ambao miongoni mwao walikuwepo Mons. José Luis del Palacio, Askofu Mstaafu wa Jimbo la Callao, Peru, Pd. Gabriel Benedicto, Askofu Msaidizi wa Madrid, Wilaya ya 6, na Pd. Eduardo Zapata, gambera wa Seminari ya Kijimbo ya Redemptoris Mater ya Mama Yetu wa Almudena.
Mkutano uliendelea katika siku nzuri sana kwenye majira ya machipuko, kwenye mazingira ya sherehe na ushirika, ambapo Kiko na Mwadhama José Cobo walizungumza kwa zamu, na katikati injili ya siku hiyo ilitangazwa (Mt 28, 16-20). Kiko alianza maneno yake kwa kumwelezea Kardinali Cobo furaha na heshima aliyoonja kwa ziara yake, akikumbuka kwa kifupi mianzo ya Njia ya Neokatekumenato na jinsi Askofu Mkuu wa Madrid wakati huo, Mh. Casimiro Morcillo, ambaye alikuwa ameteuliwa si muda mrefu uliopita, akivitembelea vibanda na kushangazwa na jumuiya aliyoikuta huko, aliwaalika kupeleka kwenye parokia maang’amuzi waliyoyaishi katika vibanda hivyo miongoni mwa maskini. Kisha alitambulisha mbele ya Don José Cobo ‘…kwa mistari michache ya mchoro…‘ -kama apendavyo kusema kwa vile ni mchoraji- hatua na mwendo halisi katika ngazi ya kiparokia wa karama hii, akimalizia kwa maneno haya:

‘Mbele ya upweke wa mwanadamu wa leo, Njia ya Neokatekumenato imeitikia jambo hili la kisosholojia kwa lingine kubwa zaidi: kuzalishwa kwa jumuiya ya kikristo kwa mfano wa Familia Takatifu ya Nazareti; jumuiya ndogo za kikristo zinazoishi katika unyenyekevu, urahisi na sifa, zinazokuwa ulimwenguni mwili unaoonekana wa Kristo Mfufuka, ambapo maneno ya Bwana huwa halisi: “Mpendane kama nilivyowapenda ninyi. Katika upendo huo watajua ya kuwa ninyi ni wanafunzi wangu”. Neokatekumenato (Ukatekumeni Mpya) nzima itakuwa ugunduzi wa Ubatizo, tukishuka ngazi za kisima cha ubatizo hatua kwa hatua hadi kuyafikia maji ya ubatizo… Tunamtangaza Yesu Kristo kuwa ndiye aliyekuja mviringo wa mauti, unowafunga kweli wanadamu wote. Mtu hawezi kupenda. Kwa nini? Kwa sababu hajashinda mauti. Mungu amemtuma Yesu Kristo kukiangamiza kifo kwa ufufuko wake.
Kardinali Cobo amelishukuru kusanyiko kwa uwepo wao na akasema:
‘Kuna kitu ambacho Kanisa limekuwa nacho tangu mwanzo. Kanisa limesema kwamba ili kujua mahali Yesu alipo na kuweza kuwaambia wengine, ni lazima kufanya mchakato fulani. Na kufanya safari na njia ili, kwa shuhuda za sisi kwa sisi, kupitia hekima ya Kanisa, tuanze kujua Yesu yuko wapi…Hicho ndicho ambacho jimbo letu la Madrid linahitaji.

Baada ya maneno haya, Kardinali aliongeza ‘maombi-shukrani’ -ndivyo alivyoziita yeye- kwa Njia ya Neokatekumenato: kujulisha jimboni mang’amuzi ya Njia kwa yahusuyo kufanya upya ubatizo; pili, kusambaza humo humo mang’amuzi thabiti ya maisha ya kijumuiya ya imani iliyotunzwa; tatu, kuendelea kufanya kazi pamoja na mikondo mingine ya kikanisa. Pamoja na kuwa mkutano rasmi wa kwanza wa Askofu Cobo pamoja na washiriki wa karama hii, jioni hiyo ilikuwa sherehe kwelikweli ambapo kondoo na mchungaji walifurahia pamoja upendo wa Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, huko wakiona maneno ya Zaburi 148 yakitimizwa: “…wavulana na wasichana, wazee pamoja na watoto…” wakati hapo hapo Jimbo Kuu la Madrid na Njia ya Neokatekumenato zimetimiza miaka 60.



