Nuru ya Bikira Maria Mkingiwa yang’aa huko Oviedo

Njia ya Neokatekumenato inaadhimisha kumbukumbu ya miaka 50 huko Oviedo (Hispania) kwa uwepo wa Kiko Argüello na Askofu Mkuu Mha. Jesús Sanz Montes. Tamasha huko Oviedo Ili kuadhimisha miaka 50 ya Njia ya Neokatekumenato huko mkoani Asturias, katika mji wa Oviedo, Askofu Mkuu Mons. Jesús Sanz Montes aliongoza Mkesha wa Sherehe ya Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili pamoja na jumuiya za Neokatekumenato za mji huo mkuu Mkoa wa Asturias.

Shahada ya Udaktari wa Hesima (“Honoris causa”) yatolewa kwa Pd. Mario Pezzi

Siku ya Alhamisi, Novemba 13, Padre Mario Pezzi, mpresbiteri wa Kikundi cha Kimataifa cha Njia ya Neokatekumenato, atapokea Shahada ya Udaktari wa Heshima ya Theolojia kutoka Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Mt. Antonio cha Murcia (UCAM). Heshima hiyo itatotelwa ndani ya hafla ya ufunguzi wa mwaka wa masomo wa 2025-2026, mbele ya Monsinyori José Manuel Lorca Planes, Askofu wa Jimbo la Cartagena-Murcia, María Dolores García Mascarell, Rais wa UCAM, Josefina

“Tuzo Maalum ya Mwaka” katika gazeti la kidijitali “Religión en Libertad” yatolewa kwa Kiko Argüello

Jumatano tarege 29 Oktoba 2025 (Madrid, Hispania) RATIBA 19:30: Mwanzo wa hafla. Utambulisho kutoka kwa Álex Navajas na Sandra Segimon. Kukabidhi tuzo: 20:45: Mwisho wa hafla na wageni waalikwa kuagwa.

Ufafanuzi wa Njia ya Neokatekumenato + Nyongeza

Njia ya Neokatekumenato ni safari ya malezi ya kikatoliki inayotekelezwa katika majimbo kupitia huduma za bure (taz. Kifungu cha 4 cha Statuta za Njia ya Neokatekumenato), iliyoidhinishwa na Kiti Kitakatifu. Mikusanyiko ya maadhimisho ya jumuiya hutumia nyenzo mbalimbali (nyimbo, ishara za kiliturujia na michoro), ambazo ni matunda ya ubunifu wa Kiko Argüello na Carmen Hernández, ambao, bila kutafuta faida, wamezifanya zipatikane bila gharama yoyote kwa ndugu wa jumuiya na parokia

Tamasha katika Kathedrali ya Cordoba, Hispania

Mateso ya wasio na hatia na Masiya, 19 Oktoba 2025 Orkestra na Kwaya ya Kisimfonia ya Njia ya Neokatekumenato ilitumbuiza huko Cordoba (Hispania), katika mazingira ya kuvutia ya Kathedrali yake, inayotambulika kwa muundo wake kama Msikiti, mbele ya kanisa lililojaa waamini na makasisi kadhaa. Miongoni mwao, waliohudhuria ni Askofu wao Mkuu, Monsinyori Jesús Fernández, pamoja na Askofu Mstaafu wa jimbo hilohilo, Monsinyori Demetrio Fernandez, na Askofu Mstaafu wa Jimbo la

Vijana 120,000 kutoka Njia ya Neokatekumenato huko Roma kwa ajili ya Jubilei na Papa na mkutano wa miito.

Kama hitimisho la Jubilei ya Vijana, iliyotakwa na Baba Mtakatifu Fransisko na kuadhimishwa na Baba Mtakatifu Leo XIV, ili kurejesha matumaini kwa dunia ya leo, vijana 120,000 kutoka jumuiya za Njia ya Neokatekumenato kutoka nchi 109 katika mabara matano wamekusanyika alasiri ya leo, tarehe 4 Agosti 2025, mahali pale pale pa mkutano na Papa, pamoja na Kikundi cha Kimataifa cha Kiko Argüello, María Ascensión na Padre Mario. Katika jukwaa kuu,