Ufunguzi wa Mchakato wa Kutangazwa Mwenye Heri na Kutangazwa Mtakatifu wa Carmen Hernández

Mubashara Kutoka Madrid (Hispania), jumapili tarehe 4 Desemba, 2022,  saa 2 usiku, East Africa Time (GMT +03:00)  Jimbo Kuu la Madrid Kituo cha michezo cha Chuo Kikuu cha Francisco Vitoria. Anaongoza ibada Kard. Carlos Osoro, Askofu Mkuu wa Madrid. Waanzilishi wa Mchakato: Kiko Argüello, P. Mario Pezzi, Ascensión Romero, Taasisi za “Familia ya Nazareti” za Roma na Madrid. Mwombaji: Carlos Metola.

Kusali kwa kupitia maombezi ya Carmen Hernández

Alizaliwa Ólvega (Soria) tarehe 24 Novemba 1930 na aliishi utotoni mwake huko Tudela (Navarra). Tangu alipokuwa mtoto, alisikia wito wa kimisionari , akivutiwa na roho ya Mt. Fransisko Ksaveri. Alisomea Sayansi za Kemia katika Chuo Kikuu cha Madrid. Kwa miaka kadhaa alikuwa sehemu ya “Taasisi ya Kimisionari ya Kristo Yesu” na alisoma Teolojia huko Valencia. Mwaka 1964 alimfahamu Kiko Argüello katika vibanda vya Palomeras Altas huko Madrid, na baada ya