Asubuhi ya leo, Jumamosi, tarehe 27 Januari 2024, Papa Fransisko aliwapokea katika hadhira binafsi Kikundi cha Kimataifa cha wajibikaji wa Njia ya Neokatekumenato: mwanzilishi Kiko Argüello, Padre Mario Pezzi na Ascensión Romero.
Katika hadhira hiyo, Kikundi walimjulisha Baba Mtakatifu kuhusu Kuishi Pamoja ya Kiulimwengu, ambayo imehitimishwa hivi punde, ikiwa na zaidi ya makatekista wasafiri 1,000, wanaowajibika kwa mataifa 136 ambapo Njia ya Neokatekumenato ipo, na Magombera wa Seminari za Kimisionari za Kijimbo Redemptoris Mater 120, na wamemsimulia walivyoishi siku hizo katika ushirika wa kina, na kuona, kupitia mang’amuzi ya makatekista wasafiri, nguvu ya Roho Mtakatifu anayetenda ndani ya ndugu wengi ambao walikuwa mbali na Kanisa na ambao wanafurahi kuwa wamekutana na upendo wa Mungu katika Yesu Kristo.
Katika mazungumzo hayo, Baba Mtakatifu amemkumbuka Mtumishi wa Mungu Carmen Hernández na amewashukuru na kuwatia moyo Kikundi katika kuendelea na kazi ya uinjilishaji popote duniani na pamoja na Seminari za Redemptoris Mater.