Njia ya Neokatekumenato na Jubilei

Ushuhuda wa Kiko Argüello. Pentekoste 2025 Naitwa Kiko Argüello na, pamoja na Mtumishi wa Mungu, Carmen Hernández, sisi ni waanzilishi wa Njia ya Neokatekumenato, utaratibu wa kijimbo wa uingizwaji wa kikristo ambao – kupitia katekesi, Neno la Mungu na sakramenti zinazoshirikiwa katika jumuiya – huwaongoza watu kuishi imani kipevu na ushirika wa kindugu. Mimi ni mchoraji mhispania. Wakati wa miaka yangu ya chuo kikuu, baada ya dhahama kubwa ya kiutu,