Kwa kumbukumbu ya Kardinali Paul Josef Cordes

Wenye shukrani kwa Mungu kwa huduma yake ya thamani katika Kanisa Alfajiri ya leo (tarehe 15 Machi, 2024) Bwana amemwita Kardinali Paul Josef Cordes kwa zawadi ya uzima wa milele. Kanisa zima, na hasa Njia ya Neokatekumenato, linamshukuru sana kwa kazi aliyoifanya kwa miaka mingi ya maisha yake, akisindikiza, kupitia ushauri wake wenye busara, kuzaliwa, kukua na kuingizwa polepole ndani ya Kanisa kwa vyama na mikondo mingi sana ya kikanisa,

Papa anampokea Kiko Argüello, mwanzilishi wa Njia ya Neokatekumenato

Asubuhi ya leo, Jumamosi, tarehe 27 Januari 2024, Papa Fransisko aliwapokea katika hadhira binafsi Kikundi cha Kimataifa cha wajibikaji wa Njia ya Neokatekumenato: mwanzilishi Kiko Argüello, Padre Mario Pezzi na Ascensión Romero. Katika hadhira hiyo, Kikundi walimjulisha Baba Mtakatifu kuhusu Kuishi Pamoja ya Kiulimwengu, ambayo imehitimishwa hivi punde, ikiwa na zaidi ya makatekista wasafiri 1,000, wanaowajibika kwa mataifa 136 ambapo Njia ya Neokatekumenato ipo, na Magombera wa Seminari za Kimisionari