Marta Obregón, shahidi wa usafi wa moyo na mfano kwa vijana

Na Javier Lozano Maandishi na picha: Jarida la Misión www.revistamision.com, makala imechapishwa katika toleo la 72. Mtumishi wa Mungu Marta Obregón alikufa akiwa tu na umri wa miaka 22, akitetea hadi mwisho jambo la thamani zaidi alilokuwa nalo: usafi wake. Ushuhuda wa msichana huyu kutoka Burgos, ambaye kwa sasa yuko kwenye mchakato wa kutangazwa kuwa mwenye heri, unaleta neema kubwa kadhaa, hasa katika ulimwengu huu wa sasa ambao hauupi mwili