Barbastro na Mashahidi wake

Wakati wa Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Hispania, Kanisa Katoliki lilipitia madhulumu makubwa, watu 10,000 waliuawa kwa imani yao. Barbastro, licha ya udogo wake, lilikuwa jimbo lenye mashahidi wengi zaidi katika Hispania nzima, 88% ya wakleri.

“Hispania imetoa “Kozi” za Ukristo, Opus Dei, Njia ya Neokatekumenato na chochote unachotaka, unajua kwa nini? , kwa sababu ilitamalaki vita vya wenyewe kwa wenyewe ambapo mapadri zaidi ya 6,000 wameuawa, walioteswa, mashahidi: hakujawa na ukengeufu hata mmoja. Mizizi ya Njia ya Neoktakumenato imeloweshwa katika damu ya mashahidi wengi wa Hispania.”

Kiko Argüello

Carmen Hernández

“Utoto wa Carmen uliwekwa alama na tukio la Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Hispania (1936-1939), vilivyotokea kati ya Tudela na Ólvega. Ulikuwa wakati mgumu kweli kweli na wa kushtusha kwa Hispania yote. Huo ulikuwa wakati wa njaa kali na, kwa upande mkubwa wa nchi, wa madhulumu ya kidini yenye kumwaga damu kwa Wakatoliki. Kwa bahati nzuri kwa familia ya Hernández, jimbo la Soria na maeneo ya jirani ya Navarra na Aragon yaliangukia mapema nyuma ya kile kinachoitwa “eneo la kitaifa”, ambako hakukuwa na madhulumu ya kidini; ingawa mwanzoni mwa mgogoro huu, karibu sana na eneo hilo kulikuwa na madhulumu ya kikatili, hasa katika jimbo la Barbastro, huko Huesca (Aragon), ambapo katika kiangazi cha 1936 watawa wengi waliuawa, wakiwemo vijana waseminari waklareti ambao walikuwepo pale, pamoja na walezi wao na askofu mwenyewe, waliouawa kishahidi/kifiadini kwa mikono ya vikundi vya wafuata utawala huria na wakomunisti vilivyotokea Catalonia.”

A. Cayuela, Carmen Hernández: Wasifu wa maisha, Madrid
Maktaba ya Waandishi wa Kikristo (BAC), 2021 (uk. 37-38)

Mashahidi Waklareti na nyumba yao ya makumbusho

Kati ya Agosti 12 na 15, 1936, Wamisionari 51 Waklareti waliuawa kwa kutokana imani yao. Walikufa wakiwasamehe waliowaua. Thelathini kati yao walikuwa kati ya miaka 21 na 23. Waliwekwa kizuizini, walinyanyaswa, hawakupewa maji wala chakula. Walitegemezwa na komunyo ya kila siku na sala. Jumba la Makumbusho la Mashahidi Waklareti wa Barbastro linawakumbuka watawa hawa. Masalia yake yanaweza kuenziwa huko.

Na kutafakari vitu vyao binafsi, barua, wosia n.k., ili kugundua ujumbe wa imani, matumaini na msamaha ambao maandiko yake yanasambaza.

Eneo la ushahidi

Wakiwa njiani kuelekea sehemu inayoitwa Eneo la ushahidi hakuna aliyeweza kuwanyamazisha. Walikwenda kifoni wakiimba wimbo wa Kiklareti: “Kwa ajili yako Mfalme wangu nitatoa damu”.

Baadhi ya maneno yao kabla ya kufa: Kristo Mfalme aishi”, “Jipeni moyo ndugu, tunateseka kwa ajili ya Kristo”, “Tunawasamehe kwa nafsi yetu yote”, “Tutaonana mbinguni”.

Mwenyeheri Florentino Asensio Barroso.

Shahidi mwingine wa Jimbo hilo alikuwa Mwenyeheri Florentino Asensio Barroso, askofu wa Barbastro, aliyekamatwa, kuteswa na kuuawa mnamo Agosti 9, 1936. Maneno yake kwa wauaji: Mnanipeleka kwenye utukufu. Ninawasamehe. Mbinguni nitawaombea.

Mashahidi wa Monasteri ya Nuestra Señora del Pueyo (Bikira Maria wa Pueyo)

Karibu na Barbastro, kwenye kilima, “Malkia wa Mbinguni” alionekana kwa mvulana mchungaji, kanisa lilikuwa lijengwe hapo. Vita pia vilifikia Monasteri ya El Pueyo. Licha ya kuweza kukimbia, watawa 18 wabenedikto waliamua kubaki. Wote waliuawa kati ya Agosti 9 na 28, 1936. Katika lori lililokuwa likiwapeleka hadi kifoni walipiga kelele: Kristo Mfalme aishi”, “Bikira wa Nguzo aishi.

Ushuhuda wa Mashahidi bado uko hai, njoo uwe shahidi!

Tarehe 25 Oktoba 1992, Wamisionari 51 Waklareti walitangazwa kuwa wenyeheri na Mtakatifu Yohane Paulo II. Sikukuu yao inaadhimishwa tarehe 13 Agosti. Papa alisema maneno haya siku hiyo kwa ajili yao : “Shuhuda zote zilizopokelewa zinaturuhusu kuthibitisha kwamba Waklareti hawa walikufa kwa ajili ya kuwa wanafunzi wa Kristo, kwa kutotaka kukana imani yao na viapo vyao vya kitawa. Kwa sababu hiyo, kwa damu yao iliyomwagika wanatutia moyo sisi sote kuishi na kufa kwa ajili ya Neno la Mungu ambalo tumeitwa kulitangaza”.


Ili kutembelea Barbastro, tuma barua pepe kwa:

Humo utaeleza siku na saa unayotamani na idadi ya wahiji.


Pakua kipeperushi (kwa kihispania)
Share: